2016-11-30 16:18:00

Ajali ya ndege yauwa watu 71: Papa atuma salam za rambi rambi!


Baba Mtakatifu Francisko ametuma salama za rambi rambi kwa Kardinali Sérgio da Rocha, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Brasilia nchini Brazil ambaye pia ni Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Brazil kutokana na ajali mbaya ya ndege iliyotokea siku ya Jumanne, tarehe 29 Novemba 2019 na kusababisha vifo vya watu 71, ikiwemo timu ya mpira wa mguu ya Chapecoense iliyokuwa inakwenda nchini Colombia ili kushiriki katika finali za mashindano ya kombe la mpira wa miguu, Amerika ya Kusini.

Salam za rambi rambi zimeandikwa kwa niaba yake na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican. Baba Mtakatifu Francisko anapenda kuziweka roho za marehemu mbele ya Uso wa huruma wa Baba wa milele pamoja na kuwaombea faraja wale wote walioguswa na kutikiswa na msiba huu mzito. Baba Mtakatifu amewapatia baraka zake za kitume pamoja na kuwaombea uponaji wa haraka wale waliojeruhiwa kutokana na ajali hii ya ndege. Taarifa zinaonesha kwamba, ndege hii ilikuwa na abiria 81, kati yao kuna watu sita ambao wamesalimika na wengine wawili hao zao bado ni tete sana. Vyombo vya ulinzi na usalama wa anga vinaendelea kuchunguza kwa kina chanjo cha ajali hii mbaya.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.