2016-11-23 15:45:00

Endelezeni mchakato wa majadiliano ya kidini!


Baba Mtakatifu Francisko kabla ya katekesi yake, Jumatano tarehe 23 Novemba 2016, alikutana na kuzungumza na washiriki wa mkutano wa kimataifa wa majadiliano ya kidini ulioandaliwa na Baraza la Kipapa la Majadiliano ya kidiniĀ  pamoja na wajumbe kutoka katika Taasisi ya Utamaduni wa Kiislam na Mahusiano kutoka Terehan nchini Iran. Baba Mtakatifu amewashukuru na kuwapongeza viongozi wakuu wa Baraza la Kipapa la Majadiliano ya kidini pamoja na wajumbe husika na kwamba, anathamini sana majadiliano ya kidini.

Baba Mtakatifu bado ana kumbukumbu alipotembelewa na Rais wa Iran, ana thamini sana utamaduni wao na kwamba, alifarijika sana kwa kutembelewa na Makamu wa Rais wa Iran aliyekuwa ameambatana na Majaalim wa kike. Aliguswa na kuridhishwa na uwepo wao. Anawashukuru na kuwapongeza kwa uwepo na ushiriki wao katika majadiliano ya kidini. Amewaomba kumkumbuka kwa sala na dua zao katika maisha na utume wake.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.