2016-10-25 08:08:00

Vatican na Serikali ya Benin watiliana sahihi mkataba wa ushirikiano!


Askofu mkuu Brian Udaigwe, Balozi wa Vatican nchini Benin, Ijumaa, tarehe 21 Oktoba 2016 ameongoza ujumbe wa Vatican katika utiaji wa sahihi kwenye hati ya Mkataba wa kisheria kuhusu Kanisa Katoliki nchini Benin. Bwana Aurèlien Agbenonci, Waziri wa Mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa Kimataifa ameongoza ujumbe wa Serikali ya Benin katika tukio hili. Mkataba una utangulizi na Ibara 19 zinazolihakikishia Kanisa Katoliki nchini Benin kuweza kutekeleza dhamana na utume wake kwa uhuru.

Serikali inatambua kisheria viongozi wa Kanisa pamoja na taasisi zake. Sehemu hizi mbili kwa kulinda na kudumisha uhuru wake, zinapenda kushirikiana kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi kasa katika nyanja za: kimaadili, kiroho na kiutu kwa ajili ya wote. Mkataba huu utaanza kutekelezwa pale pande zote mbili zitakaporidhia mkabata huu.

 

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.