2016-10-11 13:36:00

Adhabu ya kifo!


Baba Mtakatifu Francisko tarehe 10 Oktoba 2016 ameungana na Baraza la Jumuiya Ulaya kupinga adhabu ya kifo inayokwenda kinyume cha haki msingi za binadamu. Hii ni siku ambayo ilianzishwa kwenye Umoja wa Ulaya kunako mwaka 2003 na kwamba, Umoja wa Ulaya unapinga aina zote za hukumu ya kifo, kwani ni adhabu ambayo inakwenda kinyume kabisa cha utu na heshima ya binadamu aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu.

Baba Mtakatifu ameandika ujumbe wake kwenye akaunti yake ya twitter kwa kusema kwamba #No Death Penalty# kwani adhabu ya kifo haitoi tena nafasi ya matumaini kwa mtu aliyetenda kosa.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.