2016-09-30 16:47:00

Papa apita katika anga za mataifa saba wakati akielekea Georgia


Baba Mtakatifu Francisko ameanza ziara yake Kitume ya Kimataifa  ya 16, katika Jamhuri ya Geogia na Azerbaijan. Wakati akiwa safarini kuelekea Georgia, Papa alipita katika anga za mataifa saba kabla hajaingia Georgia . Katika kila nchi alikopita alipeka salaam zake kwa wakuu wa nchi na wananchi wote kwa ujumla.

Mataifa ilimopita ndege aliyokuwa akisafiria Papa ni Italia,  Corazia, Bosnia na Herzegovina, Montenegro, Serbia, Bulgaria na Uturuki nakisha Georgia yenyewe: .

Akiwa katika anga la Italia , alimuaga Rais Sergio Matarella  akisema," Kwako Mheshimiwa Rais,  ninaianza ziara yangu ya kitume kuelekea Georgia na Azerbaijan , ambako nakwenda kwa nia ya kukutana na kuzungumza na viongozi wa serikali , dini na tamaduni mbalimbali , na pia kwa nia ya  kuwaimarisha wakristo , katika   umoja na imani".  Papa alitoa salaam zake na kuomba sala za Rais  Mattarella, zimsindikize  katika ziara hii, huku akionyesha  matumaini na kuomba uwepo wa ustawi wa kiroho wa raia na jamii Italia kwa ujumla .

Bosnia na Herzegovina

“Kwako Mheshimiwa  Rais Bakir Izetbegovic , wakati nikiruka katika anga la Bosnia na Herzegovina ,kwa ajili ya  ziara yangu ya Kichungaji Georgia na Hezergovina, ninakutakia wewe na wananchi wote , matashi mema. Na ninaikumbuka ziara yangu katika taifa hili na ninawaombeeni baraka nyingi za Mwenyezi Mungu.

Montenegro

 “Kwako Mheshimiwa Rais Filip Vujanovic , ninapoita juu ya anga la Montenegro , nikiwa katika safari yangu ya kichungaji katika mataifa ya Georgia na Azxerbaijan , ninawapa salaam zangu za dhati kwako Rais na raia wote, Na ninawahakikishia sala zangu na kuombea baraka nyingi takatifu kwa taifa hili.

Serbia

Kwako Mheshimiwa Rais Tomislav Nikolic , Wakati nikiingia katika anga la Serbia nikiw anjiani kuelekea Gergia na Azerbaijan, kwa ajili ya ziara ya kichungaji, nawapeni salam zangu za dhati kwako wewe Rais na kwa raia wote na nawahakikishia sala zangu na ninaliombea taifa hili baraka nyingi .

Bulgaria

Kwako, Mheshimiwa  Rais Rosen Plevneliev  wa  Bulgaria, wakati napita katika anga la Bulgaria nikielekea Georgia na Azerbaijan katika  ziara yangu ya kichungaji , ninakusalimu wewe Rais na raia wote wa Bulgaria. Na kwa kumbukumbu za ziara yangu katika taifa hili, ninawahakikishia pia sala zanguna kuwaombeeni baraka tele .

Uturuki 

“Kwako Mheshimiwa  Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki , wakati nikipita katika anga la Uturuki niki kuelekea Geogia na Azerbaijan, pokea  salaam zangu za dhati kwako wewe na raia wote. Kwa kumbukumbu ya ziara yangu katika taifa hili , ninapenda kuwahakikishia sala zangu na ninawaoombeni nyote baraka tele. 








All the contents on this site are copyrighted ©.