2016-09-02 11:43:00

Sherehe za Jubilee ya Huruma kwa wahudumu wa kujitolea zaanza Roma


Ijumaa hii,02.09.2016, zimeanza sherehe za Jubilee ya wahudumu wa kujitolea  ikiwa pia kama utangulizi kwa tukio kubwa la Jumapili ya tarehe 4.09.2016,  ambamo Mwenye Heri Mama Tereza wa Calcutta, atatangazwa kuwa Mtakatifu na Papa Francisko, katika Ibada itakayofanyika katika Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro hapa Vatican.

Vatican ikitangaza tukio hili imesema, kufariji  wagonjwa, kuwezesha wasioweza kufanya hija na kujenga tabasamu na urafiki  kwa wanaume na wanawake wenye ulemavu, pamoja na kutoa  muda kidogo kwa ajili ya kukutana na wafungwa na walio katika hali za kukata tamaa, ni baadhi tu ya matendo ya huruma , yatakayoonyeshwa na vyombo vya habari kwa ajili ya Jubilee ya wahudumu wa kujitolea.  Maadhimisho ya siku hizi mbili tarehe 2-4 Septemba,yanafanyika chini ya  Kaulimbiu :Kuweni na Huruma.

Katika tukio hili, Papa Francisko, amemtaka  kila mmoja ashiriki katika sherehe hizi, akiwa amejawa na imani kwamba, kila mmoja anao uwezo wa kuhudumu kwa ukarimu, kama ishara halisi ya  huruma.  Na kwamba ushuhuda wa wahudumu wa kujitolea ni muhimu sana , hata kwa wale ambao hawataweza  fika Roma.

Jubilee ya wahudumu wa kujitolea , kilele chake kitakuwa siku ya Jumapili, ambamo  itapambwa na Maadhimisho ya Ibada ya Misa, kwa nia ya kumtazangaza kuwa Mtakatifu , Mwenyeheri Mama Tereza wa Calcutta, mhudumu maarufu na kioo cha katika kazi za kujitolea bila kujibakiza au kuchoka . . Aidha utakuwa ni wakati wa kuwashukuru wote wanaofanya kazi za kujitolea hasa wakati wa maafa kama matetemeko ya aridhi na mafuriko.

Kwa mujibu wa Ratiba ya Jubilee ya Wahudumu wa kujitolea ,  Ijumaa  2 Septemba  katika  makanisa mbalimbali ya hapa Roma yaliyoteuliwa,   kutakuwa na Ibada ya kuabudu Ekaristi na Sakramenti ya Upatanisho na kisha kufanya Hija ya kupita katika Milango Mitakatifu;  pia kuwawezesha mahujaji wahudumu wa kujitiolea waliofika Roma kwa ajili ya Jubilee ya Huruma, kutembea katika nyayo za  huruma za Watakatifu na wenye Heri  walioyatolewa maisha bila kujibakiza kutika utumishi wa huruma . Makanisa hayo  yametajwa kuwa Kanisa la Mwenye Heri Luigi Novarese, Kanisa la Mtakatifu Brigid la  Campo de 'Fiori la Mtaktifu la Mtakatifu Brigida, Kanisa la MtakatifuVincent Pallotti,  Basilika la Mtakatifu Francesca Romana ,Kanisa la Watakatifu Mitume  Yakobo, Kanisa la Mtakatifu  Ignatius Loyola na Kanisa la Mtakatifu  Maria Magdalena .

Siku ya pili, Jumamosi, Septemba 3, asubuhi Papa Francisko atatoa Katekesi kwa wahudumu wa kujitolea katika Uwanja wa Kanisa Kuula Mtakatifu Petro,  majira ya saa nne, ikifuatiwa na  utajiri wa shuhuda kutoka duniani kote. Nyakati za mchana utakuwa ni wakati wa maombi na tafakari.  Na Jumapili 4 Septemba, Jubilee ya wahudumu wa kujitolea itafikia kilele chake kwa Ibada ya Misa itakayoongozwa na Papa Francisko, ambamo Mwenye Heri Mama Tereza wa Calcutta anatarajiwa kutangazwa Mtakatifu. 








All the contents on this site are copyrighted ©.