2016-08-22 15:07:00

Ujumbe wa Papa kwa Sinodi ya Makanisa ya Methodisti na Valdese


Baba Mtakatifu Francisko, kama ishara ya ukaribu wake wa kiroho" alituma salamu  za matashi mema na ujumbe  wake kwa washiriki  wa Sinodi ya Makanisa  ya Methodist na Valdese, Iliyoanza Jumapili  21 -26 Agosti 2016 Torre Pellice Turin Italia . .

Hati ya Salaam na ujumbe huo imetiwa saini na Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin,kwa namna ya kipekee, Papa Francisko ametaja kwamba, anawakumbuka katika sala na maombi yake , akiomba toka kwa Mungu ,  zawadi ya kutembea katika unyofu wa moyo kuelekea ushirika kamili, katika  kushuhudia kwa ufanisi zaidi kwamba,  Kristo ni mkombozi wa watu wote. Na kwamba Ukristo ni hija ya maisha ambamo muumini anatakiwa kupiga mwendo kwa pamoja, wote  wanawake na wanaume wa leo, kueneza moyo wa Injili ya Kristo ya kuokoa, maisha ya haki na wema. .  

Kardinali  Parolin anaelezea matumaini ya Papa kwamba,  tofauti kati ya Wakatoliki na Wavaldese na Wamethodisti ,  hazizuii kutengeneza mfumo wa  ushirikiano katika uwanja wa uinjilishaji, huduma kwa maskini, wagonjwa, na wahamiaji na utunzaji wa viumbe.   Papa alimalizia ujumbe wake , kwa kuomba msaada wa Roho Mtakatifu, uweze kutoa msaada wa kuimarisha ushirikiano  na huruma ya Bwana na amani yake kwa ajili ya wote. 

Inakumbukwa mwaka  huu mwezi Marchi , kwa mara ya kwanza katika historia ya kanisa Katoliki, ujumbe maalum wa Makanisa ya Kimethodisti na Valdese walimtembelea Papa Francisko katika majengo yake ya  kitume ya Vatican. Na mwaka jana  Juni 22, 2015, Papa Francis  alitembelea  Kanisa la Valdese la  Turin,ikiwa ni mara ya kwanza kwa Kiongozi Mkuu  wa Kanisa Katoliki  kuvuka kizingiti cha Kanisa la Valdese ,  Kanisa la tangu kale lenye kuwa na wafuasi wachache hapa Italia. 








All the contents on this site are copyrighted ©.