Jumapili iliyopita, Baba Mtakatifu Francisko wakati wa sala ya Malaika wa Bwana , aliwaombea wahanga na waathirika wa shambulio la bomu la mtu aliyejilipua wakati wa sherehe ya arusi siku ya Jumamosi , kusini mwa Uturuki. Shambuli lililosababisha watu 50 kupoteza maisha na wengine wengi kujeruhiwa . Mshambuliaji huyo wa kujitoa mhanga ametajwa kuwa mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 12 au 13, na alifyatua bomu aliliokuwa amejifunga nalo kiunoni kama mkanda na baada ya kujichanganya vizuri kwenye umati mkubwa wa watu waliokuwa wakisheherekea arusi katika mji wa Gaziantep Uturuki. Wengi wa waliofariki ni Wanawake na watoto.
Akizungumza baada ya sala ya Malaika wa Bwana , mbele ya umati wa watu waliokusanyika katika Uwanja wa Kanisa Kanuu la Mtaktifu Petro Vatican, Papa Francisko alionyesha masikitiko yake kuhusu mashambulizi ya umwagaji damu, yanayotokea katika taifa pendwa la Uturuki, na aliwaalika wote wasali pamoja nae, kwa ajili ya waathirika, wahanga na majeruhi, kuwaombea zawadi ya amani ya Bwana na faraja zake kwa wote .
All the contents on this site are copyrighted ©. |