Alhamis majira ya jioni katika Kanisa Kuu la Laterani, Papa Francisko aliongoza Ibada ya MisaTakatifu iliyofuatiwa na Maandamano ya Ekaristi takatifu hadi kwenye Kanisa Kuu la Mama Maria Mkuu katikati ya Jiji la Roma, kwa ajili ya maadhimisho ya Sikukuu ya Ekaristi Takatifu, Sherehe ya Mwili na Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo, itakayofanyika katika makanisa mengi siku ya Jumapili ijayo kutokana na sababu za kichungaji, ili kuwawezesha waamini wengi kushiriki katika tafakari ya Fumbo kuu la maisha na utume wa Kanisa.
Katika homilia yake, Papa Francisko, alitafakari Ekaristi kama mzizi Mkuu wa nguvu za Kikristo, tangu mwanzo wa Ukristo na katika maisha yote ya Kanisa kama inavyodhirishwa na maisha ya watakatifu, watu mashuhuri katika kanisa waliyoyatolea maisha yao kwa upendo, katika kuhudumia mwengine , majitoleo ya maisha yasiokuwa na kujibakiza , kuleta mkate mezani kwa wale wasiokuwa navyo wake kwa waume, kama baba au mama wa familia aafanyavyo kila siku kwa familia yake. Kwa namna hio Papa aliwakumbuka Watakatifu , wazazi na Wakristo wengine wengi wanaorarua maisha yao vipandevipande katika kuhudumia wengine.
Alihoji , leo hii ni mama na baba wangapi, ambao kila siku wanachapa kazi kwa bidii ili waweze kuyakimu maisha ya kila siku, kuweka mkate kila siku juu ya meza majumbani mwao au wale ambao mioyo yao imepodeka kwa ajili ya kufanikisha watoto wao si kukua tu lakini kukua vizuri. Na ni Wakristo wagapi, kama raia wema, wameyatolea maisha yao kwa ajili ya kutetea hadhi utu wa mtu kwa binadamu wote, hasa maskini, wanyonge na wale wanaobaguliw? Wakristo hao wapi hupata nguvu za kufanya hivyo?
Papa alihoji na kutoa jibu kwamba ni katika Ekaristi, Mkate uliomegwa kwa ajili ya wote ndimo mna makazi ya upendo wa Bwana Mfufuka ,ambao hata leo hii unamegwa , wenye kuhamasisha moyo kuwapenda wengine na kuwa watu wa huruma. Katika Ekaristi mna uwezo wa Bwana Mfufuko, ambaye leo huu pia, anaumega mkate na kurudia kusema “ fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu “. Papa aliongeza kusema , hata maandamano ya Ekaristi yatakayofanyika baada ya Misa , ni kitendo kinachoonyesha kutoa chakula hiki kwa watu leo hii, ni kuumega mkate wa maisha kama ishara ya upendo wa Kristo kwa ajili ya jiji la Roma na dunia kwa ujumla.
Baada ya Ibada ya Misa , kulifanyika maandamano ya Ekaristi kutoka Kanisa Kuu la Yohana wa Laterano hadi katika Kanisa Kuu la Bikira Maria Mkuu . Maandamano yaliyokusanyika pamoja makundi ya waamini kutoka Parokia mbalimbali za Jimbo la Roma , mashirika na taasisi za Watawa, mashirika ya hisani na mshikamano wa kidugu na watu wote kwa ujumla . Maandamano yanayolega kuwashuhudia wale wasioamaini bado kwamba kiini cha fumbo la Imani ya Kikristo ni kwamba kweli Yesu yumo kweli katika maumbile ya Mkate na Mvino wakati wa maadhmisho ya Liturujia ya Ekaristi.
All the contents on this site are copyrighted ©. |