2016-05-28 14:12:00

Askofu mkuu Migliore, ateuliwa kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Russia


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Celestino Migliore kuwa Balozi mpya wa Vatican kwenye Shirikisho la Russia, kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Migliore alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Poland. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Migliore alizaliwa tarehe 1 Julai 1952. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapewa Daraja Takatifu la Upadre hapo tarehe 25 Juni 1977. Kunako mwaka 1980 akajiunga na utume wa Kidiplomasia mjini Vatican.

Tarehe 30 Oktoba, 2002 akateuliwa na Mtakatifu Yohane Paulo II kuwa Askofu mkuu na kuwekwa wakfu hapo tarehe 6 Januari 2003 kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican. Katika utume kama mwanadiplomasia wa Vatican amewahi kufanya kazi huko Angola, Marekani, Misri, China, Vietnam, Korea ya Kaskazini na hatimaye, Poland.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.