2016-05-03 15:30:00

Papa ameonya dhidi ya kuwa Wakristo wafu au Wakristo wa kutangatanga


Papa Francisko Jumanne hii katika homilía yake, ameonyesha kusikitishwa na Wakristo wengi wasiokuwa na msimamo thabiti katika imani ya kumfuata Kristo, ambao wamesahau  kwamba, Ukristo ni  kutembea katika njia  ya Yesu pekee katika maisha ya kila siku, kwa kuwa  Yesu ndiye njia ya haki  na ukweli.  Papa pia ametaja umuhimu kwa Wakristo mara kwa mara kupima mwenendo wao wa maisha kupitia sakramenti ya upatanisho , kana hatua ya kuendelea  kutembea mfululizo kwa usahihi katika njia ya Yesu. Kufanya hivyo kunasaidia kuepuka mazoea mengine yanayoweza kuwaelekeza katika  njia nyingine zenye kuongoza katika imani potofu, au njia za mkato zenye kupotosha au kuishia  njiani. Ni kiini cha tafakari  ya Papa Francisko katika homilía yake ya Ibada ya Misa kwa Jumanne hii majira ya Asubuhi , aliyoadhimisha katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta.

Tafakari ya Papa, ikivuviwa na Somo la Injili , maneno ya Yesu ayanayosema” mimi ndiyo njia”  imetahadharisha kwamba, maisha ya  imani  ni safari ya maisha  yanayopita kila siku,ambamo mna mapambano mbalimbali yanayowakabili wakristo.  Papa alisema kuonya kwamba kuna aina mbalimbali za Wafuasi wa Kristo, alirejea  wenye kuchaganya  imani na mambo mengi , mfano kundi la Wakristo waliobaki na imani iliyokufa, pia wale wenye kuwili waonekane  lakini kumbe  ndani ya mioyo mwao  hakuna kitu, wamebaki  kama mti uliopandwa bila kumwangliwa maji au kuwekewa mbolea.Watu waliobaki na imani iliyosinyaa,  ambao kwa sababu moja au nyingine wamesahau kwamba , Ni Kristo ndiye njia pekee  sahihi  katika maisha yao, kama alivyomwambia Mtakatifu Thomasi “Mimi ni njia," "yeye ambaye ameona mimi amemwona Baba ".

Papa aliendelea kuwazungumzia  waliobaki kama wafu katika Ukristo wao, akisema wakristo kama hawa ni wale wasioeleweka katika maisha ya kiroho.  Baada ya kuitembea safari ya Imani waliyoianza vyema, wakafikia mahali wakasimama badala yakusonga mbele, wapo hapo  waki0onekana kutojua wapi pa kwenda.  Na wamebaki hapo kama wafu. Mkristo kama huyo, anakaribisha upagani katika maisha yake , hataki kusonga mbele na kustawisha heri za  katika maisha yake . Anakuwa ni mtu asiyejali wala kuwa na huruma kwa wengine.  Huyu ni mfu , ni mfu kiroho . Papa alieleza na kusema kuna Wakaristo wengi walio katika kundi hili la wafu , watu wasiokuwa na imani tena ndani ya mioyo yao ingawa wanajihesabu kama ni Wakristo.  

Aidha Papa aliwazunguzia wale wanaoishi maisha ya kutangatanga katika imani. Leo wako katika kanisa na kesho wako kule, mara wanaingia dini hii na kuiacha , wenye kutangatanga na  hatima yao ni kupoteza uzuri wa kumkaribia Kristo katika njia yake maisha . Hupoteza njia , kutokana na na uzururaji mwingi unaowasababisha hata  kupoteza ukweli  na hivyo humezwa na mambo ya kidunia, yanayowanasa hata wasijue tena mlango wa kutokea. Papa amesema kundi hili halina dira  wala lengo , wapowapo tu wakifuata upepo wa marafiki na majirani, wakihama toka dhehebu moja hadi jingine, dini moja hadi nyingine. Huu ni uzuraji katika imani, jambo lisilotakiwa. Papa alieleza na kuonya kwamba,  ni lazima kama Mkristo kuacha tabia ya namna hiyo. Ni lazima kusimama imara katika njia moja tu nayo ni Yesu Kristo!.

Papa alieleza na kusema safari ya Imani ya Mkristo huanza tangu wakati wa ubatizo. Ni safari ya kiroho tunayoitembea wakati wote , kuyaacha ya dunia , kuachana na ubatili wa dunia, na kusonga mbele na yaliyo mema yenye kuleta furaha na faraja kamili  kwa kuwa tunatembea na tegemea la kukamilisha safari katika mkono wa Bwana Mbinguni . Kutembea kwa Mujibu wa Heri zilizotangazwa na Yesu Mlimani.

Papa alikamilikamisha homilía yake kwa kutoa wito kwa kila mmoja kupata muda mfupi hata wa dakika tano, kutafakari kwa jinsi gani , anaupiga mwendo wa  Maisha ya Kikristo. Ajiulize, Je nimesismama kama nguzo bila kusonga mbele huku nikifanya makosa yenye kuniyumbisha huko na kule , au usimama katika mambo ninayoyapenda bila ya kujiuliza kama yanafaa katika maisha ya Kikristo ,ambamo Yesu anasema Yeye ndiye njia ya kweli ‘. Hivyo aliomba msaada wa Roho Mtakatifu kutufundisha jinsi ya k utembea vizuri , milele na milele amina. 








All the contents on this site are copyrighted ©.