2016-05-03 15:05:00

Mons. Vayalunkal ateuliwa kuwa Balozi wa Vatican na Askofu mkuu!


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Kurian Mathew Vayalunkal kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Papua New Guinea pamoja na kumpandisha hadhi kuwa ni Askofu mkuu. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu mteule Vayalunkal, alikuwa ni mshauri kwenye Ubalozi wa Vatican. Alizaliwa huko Vadavathoor, India tarehe 4 Agosti 1966. Baada ya masomo na majiundo yake ya kipadre, akapewa Daraja Takatifu la Upadre hapo tarehe 26 Desemba 1991.

Kunako tarehe 3 Juni 1998 alijiunga na utume wa kidiplomasia mjini Vatican na kubahatika kushirikisha karama na vipaji vyake kwenye Ubalozi wa Vatican nchini Guinea, Korea Jamhuri ya Watu wa Dominican, Bangadesh, Hungaria na Misri.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.