Mapema Jumanne hii, Baba Mtakatifu Francisko aliongoza Ibada ya Misa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican, iliyoandaliwa kwa ajili ya Jumuiya ya Wafranciskani ” Ndugu Wadogo wa Mtakatifu Francisko”( Wakapuchini) , waliokusanyika Roma kutoka sehemu mbalimbali za dunia . Mkusanyiko uliolenga kutafakari kwa pamoja uhusiano na uwepo wa masalia ya Watakatifu Wawili wenzao, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Mtakatifu Pius wa Pietrocina na Mtakatifu Leopoldo wa Mandic, Wakapuchini , walioyakana maisha ya kidunia na kujiweka katika imani ya kumtumikia Kristo, kama Mapadre.
Baba Mtakatifu katika homilia yake, aliwaambia Wakapuchini hao kwamba, , anazungumza nao kama mmoja wao katika udugu wa Wakapuchini, na kupitia kwao alipenda kufikisha ujumbe wake kwa waungamishaji wote , hasa katika mwaka huu wa huruma ya Mungu , kwamba, maungamo ni kwa ajili ya kutoa msamaha kwa mwenye dhambi anayeugamana. Na hivyo muungamishaji anapaswa kutoa msamaha, na si kumpiga mjeledi wa malipizi muungamaji .
Aliongeza kuwaasa, mtu anayekuja kuungama, ni mtualiyepondeka moyo kw amakosa aliyoyafanya na hivyo anakuja tafuta faraja , kuomba msamaha, ili nafsi yake ipate kuwa na amani. Kwa hiyo, anategemea kumkuta baba aliyetayari kumkumbatia na kumwambia Mungu anakupenda. Muungamaji atapenda kumkuta Padre anayemfanya ajisikie vizuri, kujenga upya mahusiano yake yakuwa karibu na Mungu. Papa alieleza na kuonyesha kutambua kwamba, wengi wao wamesikia watu wakisema, kwa padre yule kwamwe siwezi kwenda kuungama, kwa kuwa siku moja alinifehehesha kwa maswali mengi yake, Padre yule alinifanyia hiki au kile na sasa siwezi kwenda kwake…
Baba Mtakatifu alieleza na kuwataka wote waliopewa dhamana hii ya kuwa waungamishaji na watoaji wa msamaha kwa jina la Kristo, kutopoteza thamani ya dhamana hii iliyotolewa bure kwao kama zawadi maalum toka kwa Bwana katika kusamehe. Na hivyo aliwaomba wasichoke kusamehe.
Aidha Papa alionyesha hamu yake, katika kuwaona waumngamishaji kila mahali wakiwa na mawazo mapana na nyoyo wazi ,wasiochoka kamwe kuwa vyombo vya kutoa Msamaha wa Mungu na wenye kuelewa mateso ya dhambi , kwa sababu wao pia lazima kutambua kwamba ni wenye dhambi , wanaohitaji kwanza kupata huruma ya Mungu ya kuokoa. Amewataka wote, waombe kutoka kwa Bwana neema ya kuwa mfano wa huruma ya Mungu na si kuwa mtu Mkatili. Wanapaswa kuonyesha sura ya kuwa wasamehevu, wapatanishi na watu wa amani.
Baba Mtakatifu alieleza na kukumbusha kuwa, kuna lugha nyingi katika maisha , lugha ya kuzumgumza maneno na pia kuna lugha ya vitendo. Na kwamba msamaha ni mbegu ya upendo na huruma ya Mungu . Amewaataka kama waungamishaji katika nafasi ya Yesu , aliyetoa maisha yake yote katika sala kwa muda mrefu, na pia kama walivyokuwa wenzao Mtakatifu Pio wa Pietrolcina na Mtakatifu Leopoldo , walivyotumia muda wao mwingi wakiungamisha watu nao pia wafanye kazi hiyo , kwa moyo wote , kumfukuza shetani katika mioyo ya watu.
All the contents on this site are copyrighted ©. |