2016-02-08 10:00:00

Papa awaombea wahanga wa tetemeko la ardhi Taiwan


Jumapili Papa Francisko, mara baada ya kupewa taarifa za maafa ya tetemeko la aridhi lililiotokea Tainan Taiwan lililoua watu wengi na wengine wengi kujeruhiwa au kuathirika kwa namna moja au nyingine, mara alipeleka salaam zake za  rambirambi kwa wote waliogusa na maafa  hayo ya maepma Jumamosi 06.02.2016.

Rambirambi za Papa, zilitumwa na Katibu wa Vatican, Kardinali Parolini, zimeonyesha  jinsi  , alivyopokea taarifa hiyo. Kwa masikitiko, ameomba salaam hizo ziwafikie familia za marehemu na majeruhi,  na pia ziwatie nguvu wale wanaofanya kazi ya kuokoa waliofunikwa na vifusi na pia kwa mamlaka ya kiraia.  Ameziombea Roho za Marehemu zipate kupokewa katika huruma ya Mungu. Na pia baraka na neema za Mungu ziweze kuwa  faraja na nguvu mpya kwa  waathirika wote wa janga hili. 








All the contents on this site are copyrighted ©.