2016-02-06 17:08:00

Mh. Padre Duncan Theodore Tsoke ateuliwa kuwa Askofu msaidizi!


Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Mheshimiwa Padre Duncan Theodore Tsoke, Makamu Askofu Jimbo kuu la Johannesburg, Afrika ya Kusini kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo kuu la Johanesburg. Askofu mteule alizaliwa kunako tarehe 15 Aprili 1964 huko Daveyton, Johanesburg. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi akapadrishwa tarehe 2 Desemba 1995 akiwa ni Padre wa Jimbo kuu la Johanesburg.

Askofu mteule tangu wakati huo amekuwa ni Paroko Msaidizi na mkurugenzi wa utume wa vijana Jimbo kuu la Johanesburg; mwalimu na mlezi wa Seminari ya St. Peter huko Pretoria. Kunako mwaka 2000 hadi mwaka 2009 aliteuliwa kuwa Makamu Askofu katika Uinjilishaji; Mkurugenzi msaidizi wa utume wa vijana na Paroko; msimamizi wa Parokia ya Familia Takatifu kunako mwaka 2000 hadi mwaka 2004 na Msimamizi wa Parokia ya St. Anthony Pucci kunako mwaka 2006- 2007. Kuanzia mwaka 2009 akateuliwa kuwa Makamu Askofu Jimbo kuu la Johanesburg na Paroko wa Parokia ya Familia Takatifu huko Turffontein.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.