2015-11-29 17:55:00

Siku kuu ya Mtakatifu Andrea Mtume!


Kardinali Kurt Koch, Rais wa Baraza la Kipapa linalohamasisha Umoja wa Wakristo anaongoza ujumbe wa Vatican kwenye maadhimisho ya Siku kuu ya Mtakatifu Andrea, Msimamizi wa Kanisa la Kiorthodox la Costantinopoli, inayoadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 30 Novemba. Ujumbe huu unashiriki katika mkesha na hatimaye Liturujia Takatifu ikayoongozwa na Patriaki Bartolomeo wa kwanza kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Giorgio al Fanar.

Ujumbe wa Vatican ulipoawasili umefanyika mazunguzmo na Patriaki Bartolomeo wa kwanza na kuwasilisha salam na matashi mema kutoka kwa Baba Mtakatifu Francisko ambaye kwa wakti huu anafanya hija ya kitume Barani Afrika. Ujumbe huu ni mwendelezo wa Mapokeo ya urafiki kati ya Makanisa haya mawili kwani wakati wa Siku kuu ya watakatifu Petro na Paulo, miamba wa imani, Patriaki Bartolomeo wa kwanza huwa anatuma ujumbe kwa ajili ya maadhimisho haya. Itakumbukwa kwamba, mwaka jana, Baba Mtakatifu Francisko alihudhuria Ibada ya Liturujia huko Istanbul, Uturuki.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.