2015-10-03 15:57:00

Papa: Ibilisi anapanda mbegu ya ubaya, ambayo hataki kamwe pawepo mbegu ya amani


Jumamosi Octoba 3 Papa Francis aliadhimisha misa na maaskari wanaosaidia kulinda usalama wa Mjini Vatican wakiwa wanafanya kumbukumbu ya Siku ya malaika mkuu Michael ambaye ni msimamizi wao iliyofikia kilele chake Septemba 30, 2015.

Akitafakari neno la Mungu kutoka katika kitabu cha ufunuo, alielezea neno la nguvu. “Ikatokea vita mbinguni” na kusema vita hivi vilikuwa vya namna gani , vilikuwa vita vya mwisho kati ya malaika wa Mungu waliokuwa wakiongozwa na Malaika Mkuu Michael dhidi ya shetani, joka kuu la zamani yaani ibilisi.

Mwisho wa matokeo ya vita hivyo lakini ilikuwa ni amani isiyo na mwisho kwa watoto wa Mungu waliobaki waaminifu. Lakini papa Francis albainisha ya kwamba licha ya vita hivyo vilivyokuwa vikifanyika, hata leo hii vita hivyo vinaendelea kufanyika kila siku , katika mioyo ya binadamu, ya wanaume na wanawake, katika mioyo ya wakristo na wasiyo wakristo. Papa alifafanua ya kwamba kuna vita kati ya wema na ubaya ambapo sisi hatuna budi kuchagua nini tunataka ubaya au wema.

Papa alibainisha ya kwamba lakini mbinu za vita hivyo kati ya maadui wawili ni tofauti.na kwamba Mbinu ya kwanza  ni ile ya sala iliyokuwa ya mwanzo wa ibada ya misa ambapo ilionekana neema ya ulinzi kutokana na Malaika Michael anayepamabana na ubaya wa ibilisi. Ibilisi anapanda mbegu ya ubaya, ambayo hataki kamwe pawepo mbegu ya amani ya maisha ya umoja, bali daima anataka ubaya , kwani ndiyo njia yake ya kupanda ubaya.Papa alisema hii inahitaji kusali hili Bwana atulinde dhidi ya ubaya huo.

Aina nyingine ya kufanya vita papa alisema ni ulaghai, kwani anayepanda ubaya ni mlaghai, maana analaghai kwa sura ya uzuri wa kiibilisi na kutufanya kuamini yote.Yeye anatambua kuuza huo uzuri wake anauza vema , lakini mwisho wake ni kulipa vibaya, na hiyo ndiyo mbinu yake. Papa aliwakumbusha jinsi Injili inavyoonyesha huyo Bwana ibilisi alivyojitokeza kwenye jangwa, wakati Yesu anasali na kufunga kwa siku arobaini, amechoka na ana njaa.Yeye alifika kwa pole kama nyoka, na kumjaribu Yesu, kama ni mwana wa Mungu, ahukumu mawe yawe mkate, kwa maana hiyo wewe kama ni mwana wa Mungu kwanini usumbuke hivyo? kama weweni mwana wa Mungu, jitupe chini kwa maana watu wote wataona huo muujiza bila kuangaika na utatambuliwa ya kwamba wewe ni mwana wa Mungu. Ibilisi alijaribu kumlaghai lakini hakashindwa , na ndipo aliamaua kumweleza nitakupa utawala wa dunia nzima ukinisujudia mimi.

Aidha papa alielezea ngazi tatu za mbinu ya nyoka wa zamani na shetani: ya kwamba  ni vitu  kwa maana hiyo  mkate, na pia utajiri, ambao taratibu unaleta rushwa , na rushwa hiyo siyo simulizi, bali rushwa ipo mahali popote papa alisisitiza.Kwa fedha kidogo watu wengi wanauza roho, wanauza furaha wanauza maisha, wanauza kila kitu. Kwa njia hiyo ngazi ya kwanza ni fedha na utajiri.Ukiwa na fedha hizo unajisikia wewe ni muhimu. Na Ngazi ya pili ni majivuno,kama yale yalioonkeka kwa ibilisi alipomwambia. Yesu Twende juu ya kinara cha ekalu na jirushe chini, ufanye maonyesho: ni kuishi kimajivuno

Na ngazi ya tatu ni ukubwa, ukiburi na kujisifu, yaani mimi nitakupatia utawala wa ulimwengu, wewe utakuwa mwenye amri.Papa aliendelea kuwaeleza ya kwamba hali hiyo inajitokeza daima kwetu kwenye mambo madogomadogo, yakushikiria utajiri, ya kupenda kusifiwa kama tausi. Watu wengi ni vichekesho. Mjivuno yanatufanya tuwe vichekesho  na unapopewa sifa na utawala  unajisikia kuwa Mungu, na hii ni dhambi kubwa papa alisema.

Papa aliendelea kusema na hayo ndiyo mapambano yetu ambayo tunapaswa kuomba Bwana kwa maombezi ya Malaika Mkuu Michael aweze kutukinga na ubaya wa shetani na kutukinga na ulaghai wa joka ambalo linaitwa shetani.Aliwambia pia kwamba wanafanya kazi kidogo ngumu ambayo daima wakumbana na mitafaruko ambapo wanapaswa waweke sawa mambo hayo ili kuzuia uhalifu au hatia, ya kwamba wanapaswa kusali sana kwa Bwana ili kwa maombezi ya  Malaika Mkuu Michael awalinde  na kila aiana ya vishawishi vya fedha au rushwa, mali, majivuno, na ukiburi.na kama watakuwa wanyeyekevu kama Yesu ndivyo hata huduma yao itazaa matunda na kuwa ya manufaa kwa wote.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.