2015-10-02 17:25:00

Papa:Kila mmoja anaye Malaika wake mlinzi, tumsikilize kwa makini


Vatican Radio:  Mungu alimpatia kila mmoja mwenzake wa kumsindikiza, ambaye ni malaika kwaajili ya kushauri na kulinda na pia Malaika ni wa kusikilizwa kwa makini.

 Papa Francis aliyasema hayo katika mahubiri yake  Ijumaa 2 Oktaba  katika Kanisa la Mtakatifu Marta Vatican ambapo,Kanisa likiwa linafanya kumbukumbu ya malaika walinzi.Papa alisema ya kwamba, ukitaka kutambua baba ambaye anapenda na pia  anafunika , anaonekana katika kurasa za kwanza za Biblia ambamo Mungu alipowafukuza Adamu na Eva katika bustani ya Eden lakini hakuwaacha peke yao na kuwaambia  fanyeni mnavyotaka.

Papa Francis anataja sala ya Zaburi ambayo inaonyesha ya kwamba malaika daima walivyo walinzi katika kila aina ya jambo lolote la binadamu na mbinguni. Bwana alimpatia Kila mmoja mwenza anaye muongoza  , na daima yupo nasi  na ni hali halisi ya kweli,  ni kama balozi wa Mungu kwetu sisi.Na Mungu anatushauri kuwa makini na kugundua uwepo wake , hata kama sisi tukiwaza kutenda ukatili na kufikiri tuko peke yetu si kweli , kwa maana yupo malaika .

Ni lazima kumsikiliza kwa makini sauti yake kwasababu anatushauri . Papa alisema, mara kwa amara tunapoijiwa na mawazo ya kufanya jambo fulani au kujisikia usifanye  ni lazima kusikiliza na wala siyo kuwa wakaidi. Aliongeza  ya kwamba Malaika  walinzi wanatutetea daima na zaidi juu  ya ubaya, na kubainisha pia  mara nyingi tunafikiria kwamba tunaweza kuficha  mambo mengi , na mambo mabaya ambayo mwisho wake lakini  hayo yote yatajitokeza kwenye mwanga.

Malaika yupo kutushuauri na kutufunika ni kama vile ambavyo anagefanya rafiki yetu ambaye mara nyingi hatumwoni lakini tunamsikia , ni rafiki ambaye siku moja atakuwa na sisi katika furaha ya milele huko mbinguni.

 Rafiki huyo lakini anahitaji usikivu , msindikizaji huyo ni wa kuheshimu na kusikilizwa  katika safari yetu anaitwa usikivu kwa makini.Kila Mkristo anapaswa kuwa makini katika usikivu  wa roho mtakatifu, Na usikivu wa roho mtakatifu  unaanza pale kwenye usikivu wa ushauri wa huyo mwenza wetu katika safari. Ili kuwa wasikivu , papa anaelekeza ni lazima kugeuka watoto wadogo, ambao Yesu mwenyewe alisema ndiyo walio wakubwa katika ufalme wa Baba yake.

Na hivyo papa alimalizia akisema ya kwamaba Malaika walinzi ni wenza wa safari ambao wanatufundisha unyenyekevu, kama vile watoto wanavyotakiwa kusikilizwa. Na tuombe neema ya Bwanan ya kuwa wasikivu , wa kusikiliza sauti ya huyo mwenza wetu  , na baloz i wa Mungu aliye karibu nasi kwa jina lake, na sisi tunapata msaada kutoka kwake.

 

 

 

 

 

 

 

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.