Vijana elfu 20 kutoka katika majimbo 21 ya nchi walifika katika adhimisho la 8 ya siku ya kitaifa ya vijana. Tukio hilo lilianza na tamasha mbalimbali kuanzia Septemba 16 -20 katika jimbo la Fianarantsoa kusini mashariki mwa Madagascar.
Mgeni rasmi wa kufungua siku hiyo alikuwa Rais wa nchi Bwana Hery Rajaonarimampianina,
wakiwemo viongozi mbalimbali wa serikali ambapo alitoa wito kwa vijana kujenga dunia
mpya na kupambana dhidi ya vurugu.
Vijana hao walipata kuigiza mchezo uliokuwa na tafakari juu ya injili ya Mtakatifu
(Matayo 5,3) usemao Heri masikini wa roho maana hao watairithi nchi.
Misa ya ufunguzi huo iliadhimishwa na Askofu Mkuu wa Fianarantsoa, Fulgence Rabemahafaly,akiwa
na maaskofu wenzake, mapadre na jumuiya nzima ya Kanisa la Madagascar.
All the contents on this site are copyrighted ©. |