2015-09-18 14:32:00

KCCB- Mikakati ya mawasiliano kwa ajili ya ujio wa Papa Francisko nchini Kenya


Kamati ndogo ya Tume ya Mawasiliano na Matangazo ya Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya, imetoa baadhi ya mikakati  mbinu, kwa ajili ya maandalizi ya ziara ya  Papa Francisko nchini Kenya,  mwezi Novemba mwaka huu.

Akizungumza na AMECEA Online News, Mratibu wa Mawasiliano wa KCCB, David Omwoyo amesema kuwa tovuti maalum kwa ajili ya ziara ya Papa itazinduliwa katika siku chache zijazo. Na pia hivi karibuni , nembo  ya ziara ya Papa itazinduliwa hivi karibuni. Nembo hiyo ina  alama  4 muhimu zinaashiria mada mbiu ya ziara : "Simama imara katika Imani ... Usiogope". Vitu hivyo vinne ni Njiwa  kama alama ya amani, moto katika nafasi ya  Roho Mtakatifu , ramani ya Kenya na Msalaba ambayo ni ishara ya Kanisa.

Na kwamba, kwa ajili ya kuwaandaa watu , katika kipindi hiki cha kusubiri ujio wa Papa , Kamati ndogo ya Mawasiliano imeunda mpango mpya wa utendaji  kwa miradi maalum, inayolenga kufanikishaji wa ziara ya Papa  kiroho na kijamii. Miradi inayoendeshwa na Kanisa Katoliki Kenya ambayo itatagazwa kupitia vituo vya Televisheni . Na Kutakuwa na mengi yatakayotangazwa na vyombo vya habari kwa wakati huu. Na kwamba, Taarifa zote zitakuwa zinapatikana katika tovuti mpya itakayozinduliwa hivi karibuni, ikiwa wazi kwa mtu yeyote ambaye anayetaka kupata habarii za ujio wa Papa Kenya. Papa Francisko anatazamia kutembelea Kenya, Uganda na Jamhuri ya Afrika Kati ,  mwezi Novemba mwaka huu. 
 








All the contents on this site are copyrighted ©.