2015-09-06 11:20:00

Vatican:Kongamano la Dunia la watawa vijana wa kike na kiume Roma


Watawa vijana wapatao 4, 000 wanawake kwa wanaume , wanategemewa kuwasili Roma kutoka pande zote za Dunia kwenye Mkutano wa   Dunia  kuanzia 15-19 Septemba .

Mkutano huo ukiwa na kauli mbiu “Amsheni Dunia - katika kuinjilisha, ki unabii na matumaini”.,  umeandaliwa na Baraza la Mashirika ya kitawa na Taasisi za vyama vya maisha ya kitume kwa  dhana  ya mwaka wa kitawa unaolendelea kuadhimishwa hadi utakapofungwa tarehe 2 Februari 2016.

Madhumuni ya mkutano huo ni kufanya uzoefu wa tafakari ya kiteolojia  kwa njia ya Biblia takatifu, kuona karama ya kiteolojia  na ya Kanisa , misingi muhimu ya maisha ya kitawa, kuwawezesha washiriki  washirikishane hali halisi ya shahuku na matarajio yao katika nyumba za malezi, vilevile ni pamoja na kusheherekea  na kushuhudia uzuri wa wito wao wenyewe.

Ratiba inasema kuwa kila siku asubuhi washiriki watakusanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Paul VI mjini Vatican, kusikiliza mada zitakazokuwa zingusa juu ya miito, maisha ya kundugu na na Utume. Mchana  watagawanyika kulingana na lugha zao kwenye maeneo yaliyoandaliwa Roma, ambapo washiriki hao watakuwa na  fursa ya kushirikishana kwa kutoa  maoni . Usiku wataweza kuchagua sehemu ya kutembelea kama vile, ya safari ya kitume , itakayofanyika katika kituo cha wamisonari, Roma, pia safari  kukutana itakayofanyika katika vituo vya Caritas Jumuiya ya Sant Egido, na Talitha Kum na  kundi la safari nzuri hiyo itakuwa ni ziara ya kutembelea  majumba ya makumbusho ya Vatican na Kanisa la Sistina.

Mpango huo ni pamoja na matukio matatu ambayo yanashirikisha watu wote ambayo ni Mkesha katika viwanja vya Mtakatifu Petro utakoongozwa na Katibu wa Mashrika kwaajili ya Tassisi ya Watawa na Vyama vya Maisha ya kitume Askofu José Rodríguez Carballo, (FM ) 15Septemba saa 2.30 Usiku.

18 Septemba  saa 2.30 kutakuwa na  tamasha la muziki na shuhuda mbalimbali katika viwanja vya Mtakatifu Petro. 19 Septemba Misa  Takatifu  katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro itakayoongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mashrika ya Kitawa na Kazi za Kitume , Kardinali Joao Braz de Aviz  saa 5:30.

Jumamosi Septemba 19 kutakuwa na sherehe ya kumbukumbu ya Watakatifu na mashahidi wa maisha ya wakfu,  itakayofanyika kuanza na maandamano, kwa sala na maombi kuanzia Kanisa la Mtakatifu Maria Aracoel na kuzunguka  hadi kufika Coliseum mjini Roma.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.