2015-08-28 16:14:00

Mwaka wa Huruma ya Mungu Mapadre waalikwa kujiunga na utume wa kimisionari


Katika adhimisho la Mwaka Mtakatifu wa Jubilee ya Huruma ya Mungu ambalo linaanza Desemba 8,2015,   katika adhimisho la Jumatano ya Majivu, Papa Francisko,  atawapeleka Mapadre walioomba kujiunga katika utume kama Wamisionari wa huruma ya Mungu, sehemu mbalimbali za dunia.

Baraza la Kipapa kwa ajili ya  ukuzaji  Uinjilishaji Mpya ,  kwa sasa linapokea maombi  kutoka kwa Mapadre wanaotaka kujiunga katika utume  huu wa kimisionari. Taarifa inasema , Mapadre hao watapewa dhamana ya kusamehe dhambi ambazo zilitakiwa kusamehewa na Kiti Kitakatifu tu. Baba Mtakatifu alieleza hilo katika barua yake ya" Misericordiae Vultus”,  waraka uliotangaza rasmi Mwaka Mtakatifu wa Jubilee ya Huruma.

Waraka huo pia ulitaja sifa za mwombaji  kukubalika kwamba, ni  ni lazima maisha yake yaashirie ishara hai ya Baba anayepokea watu wote wanaotafuta msamaha wa Mungu. -awe ni mwenye mvuto wa kuwawezesha wote , bila kubagua mtu yeyote, kukutana kweli na mtu, kama  chanzo cha ukombozi, unaotajirishwa na uwajibikaji katika kuondokana na vikwazo na kuchukua tena  maisha mapya ya Ubatizo. Awe ni Padre anayeongozwa  na maneno, "Kwa maana Mungu amewatoa  wote katika uasi , ili wote waweze kupata huruma yake; Awe ni mtu mwenye kuvuvia mahubiri wa Huruma ya Mungu , na mpiga mbiu ya furaha ya kusamehewa. Mwenye  roho nyepesi iliyojaa  upendo na huruma katika kuwapokea  waungamaji , na hasa kuwa mwangalifu zaidi katika kujali mazingira magumu yanayo mkabili  kila muungamaji.

Aidha waraka unaeleza kwamba, Wamisionari  hao wapya watapelekwa majimboni kwa mwaliko wa  Askofu wa Jimbo, kulingana na mahitaji  yake, ndani ya eneo lake, kwa ajili ya kazi za kitume au ufanikishaji wa lengo maalum lilioandaliwa kwa ajili ya jubilee hii  , na hasa kwa namna ya kipekee,  umakini wa kutoa Sakramenti ya upatanisho.  

Padre anayependa kujiunga na Utume huu wakati wa Mwaka wa Jubilee,  anashauriwa kwamba ni lazima awe na barua inayo mpendekeza kutoka  kwa Askofu wake au Mkuu wa Shirika ,  ambayo itaonyesha lengo na nia uwepo wa Padre huyo. .

Mapadre mnaopemba kujiunga katika utume huu mnaweza kutuma maombi yenu kupitia njia ya Mtandao :http://www.im.va/content/gdm/en/partecipa/missionari.html

Katika adhimisho la Jubilee ya Huruma ya Mungu ambayo tunaianza Desemba 8,  katika adhimisho la Jumatano ya Majivu, Papa Francisko,  atapeleka mapadre walioomba kutumikia kama wamisionari wa huruma ya Mungu, sehemu mbalimbali za dunia.

Baraza la Kipapa kwa ajili ya  ukuzaji  wa shughuli za Uinjilishaji,  kwa sasa linapokea maombi  kutoka kwa Mapadre wanaotaka kujiunga katika utume  huu wa kuwa wamisionari. Taarifa inasema , Mapadre hao watapewa dhamana ya kusamehe dhambi ambazo zilitakiwa kusamehewa na Kiti Kitakatifu tu. Baba Mtakatifu alieleza hilo katika barua yake ya “Sura ya Huruma”” Misericordiae Vultus”,  waraka uliotangaza rasmi Mwaka Mtakatifu wa Jubilee ya Huruma.

Waraka huo pia ulitaja sifa za mwombaji  kukubalika kwamba, ni  ni lazima maisha yake yawe Ishara hai ya Baba anayepokea watu wote wanaotafuta msamaha wa Mungu.
-awe ni mwenye mvuto wa kuwawezesha wote , bila kubagua mtu yeyote, kukutana kweli na mtu, kama  chanzo cha ukombozi, unaotajirishwa na uwajibikaji katika kuondokana na vikwazo na kuchukua tena  maisha mapya ya Ubatizo;
- Kwa kuongozwa na maneno, "Kwa maana Mungu amewatoa  wote katika uasi , ili wote waweze kupata huruma yake; 

Awe ni mtu mwenye kuvuvia mahubiri wa Huruma ya Mungu , na mpiga mbiu ya furaha ya kusamehewa. Mwenye  roho nyepesi iliyojaa  upendo na huruma katika kuwapokea  waungamaji , na hasa kuwa mwangalifu zaidi katika kujali mazingira magumu yanayo mkabili  kila muungamaji.

Aidha waraka unaeleza kwamba, Wamisionari  hao wapya wataalikwa na Askofu wa Jimbo, kulingana na mahitaji  ndani ya eneo lake,  kwa ajili ya kazi za kitume au ufanikishaji wa lengo maalum lilioandaliwa kwa ajili ya jubilee , na hasa kwa namna ya kipekee,  umakini wa kutoa Sakramenti ya upatanisho.  

Padre anayependa kujiunga na Utume huu wakati wa Mwaka wa Jubilee,  anashauriwa kwamba ni lazima awe na barua ya mapendekezo kutoka  kwa Askofu wake au Mkuu wa Shirika ,  ambayo itaonyesha  uwepo wa Padre huyo kwa  lengo fulani.

Mapadre wanaopenda kujiunga katika utume huu mnaweza kutuma maombi yenu kupitia njia ya Mtandao :http://www.im.va/content/gdm/en/partecipa/missionari.html. 








All the contents on this site are copyrighted ©.