2015-08-24 15:16:00

Utabiri wa mvua za El Nino kutarajiwa katika nchi za Afrika Mashariki


Mojawapo ya mvua kubwa Itwayo El Nino inatarajiwa kunyesha nchi za Afrika mashariki, ambayo uleta mafuriko na magonjwa kama maleria.

Hayo yameelezwa wataalumu wa hali ya hewa wa huko kenya , ya kuwa Mvua hizi ziitwazo El Nino zimeleta wasiwasi mkubwa wa hali ya hewa  kwa 1997  watu wengi walipoteza maisha yao na  kuacha maelfu ya watu bila makazi.

Wanasayansi wanasema hali hiyo ina uzoefu karibia dunia nzima ambapo inawezekana ikawa ya nguvu kunyesha  tangu miaka ya  1950.

Taarifa zinazema, wiki hii Wataalam wa hali ya hewa kutoka nchi za Afrika ya mashariki watakutana mjini Dar es salaam Tanzania kujadili matukio na uwezekano wa kukabiliana na maafa hayo. Vilevile Mashirika ya hali ya hewa duniani kote wamedhitibisha juu ya tukio linaweza  kutokea miezi ya hivi karibuni.

Wiki iliyopita Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Hali ya Hewa Ayub Shaka  wa Kenya alisema wakenya wanapaswa kusubiri taarifa zitokazo kwenye mkutano Dar Es Salaam Tanzania  juu ya utabiri wa tukio  la El Nino, japokuwa utabiri duniani kote unaonyesha uwezekano  mkubwa wa El Nino kutokea miezi ijayo  hadi mapema 2016.

 Na Shirika la Afya Duniani na Shirika la Taassisi ya utafiti wa Hali ya Hewa na Jamii katika Chuo kikuu cha Columbia  wantoa onyo juu ya kuzuka kwa malaria kwasababu ya kunyesha  mvua  nyingi na joto ya hali ya hewa, hata hivyo itabidi kufuatilia mvua hizo zenye  mafuriko.








All the contents on this site are copyrighted ©.