2015-08-24 15:01:00

Marekebisho mapya kwa mfumo wa fedha Vatican ni hatari nyingine kwa kanisa


Kardinali George Pell, Mkuu wa Sekretariati ya Uchumi katika Jimbo la Papa, ametahadharisha kwamba, marekebisho katika kanuni na  mfumo wa fedha na uchumi katika taasisi ya fedha ya Vatican, yanaweza zua shambulio jipya kwa Kanisa, kutokana na ukweli unaolenga kurekebisha makosa ya kifedha ya nyuma.  Kardinali Pell alitahadharisha hilo wakati wa majadiliano ya Jumamosi usiku katika Mkutano Rimini,  juu ya "Kanisa na fedha. Kardinali Pell alikiri kuwa ufanikishaji wa lengo la kurekebisha kanuni na mfumo wa fedha ni kazi ngumu kwa Vatican lakini ni muhimu kufanyika.  

Kardinali alieleza nia za Vatican kufanya marekebisho kwamba, inalenga kuweka kivitendo mafundisho ya Kikristo,  juu ya usimamizi wa mali na utajiri wa kanisa, katika utume wake wa Kiinjili  na hasa katika kuwatumikia watu maskini na wateswa, kwa ajili ya mahitaji kwa yote mawili kiroho na kimwili pia. Na kwamba mbinu za sasa za uhasibu ni nzuri, lakini zinahitaji  ujuzi wa kitaalam na uwajibikaji kwa mifumo iliyopitishwa ya  kanuni ya uwazi katika fedha. Mali za Kanisa ni lazima  kutumika kama mfuko wa kufadhili matendo mema ya Kanisa.

Kardinali Pell alieleza na kuonyesha kutambua, wasiwasi uliopo juu ya usimamizi wa mali na fedha za kanisa, akisema ni muhimu katika mahitaji ya  kichungaji  kwa watu, na hivyo ni lazima lipewe uzito wake kama hitaji msingi katika taratibu za kanisa za kuwekeza fedha na kumiliki mali. Hivyo kwa utawala wa kanisa,  inakuwa na wajibu wa kimaadili kuhakikisha fedha na mali vinatumika ipasavyo.  Pale panapokuwa na ufinyangaji katika matumizi maana yake kuna wanaofaidika kichinichini kwa mgongo wa walengwa katika matumizi hayo na hasa watu maskini. "Na pia ni muhimu kwa taasisi kutofautisha fedha zinazotolewa kwa kwa jina la Kanisa au katika kufanikishaji  wa uchumi wa Kanisa. Alitolewa mfano, si halali kwa Paroko kuona mema yanayotolewa kwa ajili ya Parokia kuwa ni mali yake. 

Kardinali Pell alieleza kwa kutoa mfano wa Paroko mmoja wa Australia, aliyekodisha nyumba kwa rafiki yake katika kiwango cha chini ya kiwango cha malipo ya nyumba za kupanga katika eneo hilo. Alisema kufanya hivyo ni makosa kimaadili. Alifafanua ni hatari na vibaya kimaadili, kwa kuwa ni kugandamiza haki ya mtu katika usimamizi wa fedha za Kanisa. Alihoji je  Paroko huyo akihamishwa na kuja mwingine, itakuwa halali au hapana kwa mwenye nyumba kudai malipo ya haki? Hili linaweza zua mzozo usiokuwa wa lazima ndani ya Parokia. Hari daima kusimama katika ukweli na uwazi katika kusimamia fedha.  Na kwamba meneja wa Kanisa, si lazima kuwa mtaalam, lakini lazima awe na uwezo wa kutambua mabaya katika usimamizi wa fedha, alisisitiza Kardinali Pell wa Australia.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.