Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Makada Yohannes, Afisa mawasiliano na mahusiano ya umma katika Baraza la Maaskofu Katoliki Ethiopia, Kanisa Katoliki nchini Ethiopia, limeiomba Tume ya Umoja wa Afrika (AUC) kumwalika Baba Mtakatifu Francisko, atembelee Umoja wa Afrika. Kardinali Berhaneyesus Sourapiel, Askofu Mkuu wa Addis Ababa, na Mwenyekiti wa AMECEA, alipendekeza hilo wakati wa majadiliano ya ujumbe wa Kanisa ulipokutana na Mwenyekiti wa Tume ya AUC , Dk Dlamini Zuma Nkozasana.
Kardinali Berhaneyesus na ujumbe wake walikutana na Dk Zuma kujadili masuala yanayolenga
kuimarisha uhusiano kati ya Kanisa na Tume ya Umoja wa Afrika na nchi. Ujumbe wa
viongozi wa Kanisa Katoliki, ulikiwa pamoja na Dk Berhane Gebray ambaye ni Mwenyekiti
kwa kamati ya maandalizi ya Mkutano wa 19 wa AMECEA, mkutano utakaofanyika nchini
Ethiopia mwaka 2018. Katika majadiliano yao walitoa pia mapendekezo ya jinsi AUC inavyo
weza kushirikiana na Kanisa Katoliki katika maandalizi ya mkutano huo.
Kwa upande wake Dk Zuma alisema kuwa itakuwa ni heshima kubwa kumkaribisha Papa Francisko.
Lakini ni lazima kufanya kazi kwa pamoja, Kanisa Katoliki nchini Ethiopia na Serikali
ya Ethiopia, na AUC kushirikishwa katika vikao na maandalizi yake. Ilikubaliwa
kuwa kikundi cha kufuatilia hilo kitaundwa. Katika majadiliano yao pia ilikubalika
kuteuliwa kwa Kasisi wa Kudumu kwa ajili ya kazi za kichungaji kwa wafanyakazi katika
Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika. Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Kardinali
Berhaneyesus kuitembelea Tume ya Umoja wa Afrika , tangu alipochaguliwa kuwa Kardinali.
Makeda Yonannes wa CBCE ameripoti .
All the contents on this site are copyrighted ©. |