2015-08-14 16:21:00

Jitihada za Umoja wa Mataifa dhidi ya mlipuko wa Ebola Africa


Alhamis 13Agosti Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa , lilikutana kuhusu amani na usalama barani Afrika likitioa mtazamo wake juu ya jitiada za kimataifa dhidi ya mlipuko wa homa ya virus vya Ebola. Mkutano huo ulifanyika kwa njia ya Video na Mkurugenzi  Mkuu wa Shirikala Afya Duniani, Bi Margaret Chan, akiwa Hong Kong na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu kuhusu Ebola Bwana David Nabarro akiwa Geneva .

Katika hotuba yake, Bi Margaret Chan alisisitiza umuhimu wa hatua zilizopigwa katika kukabiliana na Ebola  katika nchi ya Guine na Sierra Leone na  kwamba zimeripotiwa visa vitatu tu katika kipindi cha wiki mbili zilizopita. Zaidi ya hayo alitoa onyo la kutokulegeza umakini, akitoa mifano ya kisa kimoja ambacho akikugunduliwa kutokana na kutoroka kwa mtu mmoja kuroka kituo cha afya, au kisa kingine cha kufanya mazishi yasiyo salama yanaweza kuibua visa vingine vya ebola.

Naye Daktari Nabarro alitoa msisitizo muhimu wa  kuhusisha jamii latika jitihada za kukakabiliana na mlipuko  akisema kuwa kutokana na kwamba ;Hofu ya watu inakabiliwa kwa urahisi, tamaduni muhimu zinafanywa kuwa salama na kuheshimiwa, mitandao ya maambukizi inagundulika haraka, waliokaribiana na wagonjwa wanatambuliwa haraka na mlipuko unamalizika haraka zaidi.

Tanzania:

Na habari nyingine kuhusu Ebola kutoka shirika la kuhudumia wakimbizi UHCR na shirika la Afya Duniani WHO , yametoa wito wa utulivu kufuatia ripoti za kifo cha mkimbizi wa Burundi kinachoshukiwa kutokana na kirusi cha Ebola, mnamo Agosti 10 2015.

Mkimbizi huyo ambaye alikuwa ameishi katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu kwa muda wa miaka mitatu akisubiri kuhamishiwa Marekani, alifariki dunia katika hospitali ya Maweni katika mkoa wa Kigoma, Kaskazini Magharibi mwa Tanzania.

Mnamo Agosti 9, mkimbizi huyo alipelekwa kwa hospitali ya Maweni, akiwa anatokwa damu katika ufizi, macho na masikio. Alikuwa pia amechoka, huku mwili ukiwasha, ingawa hakuwa na homa. Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Alvaro Rodriguez

Ripoti zinasema kwamba  Bwana Alvaro ameliambia shirika la habari la Umoja wa mataifa kwamba uwezekano kuwa ni Ebola ni mdogo, hata hivyo Tanzania imejitayarisha kukabiliana na mlipuko wa aina hiyo.








All the contents on this site are copyrighted ©.