Mkutano wa Wakristo Wafanyakazi walenga katika kujenga mshikamano na udugu endelevu katika mwa jamii
"Kujenga jamii ya haki, udugu endelevu ni hoja inayotazamwa kwa makini na Mkutano wa Chama cha Wakristo Wafanyakazi, uliofanyika mjini Ouagadougou Burkina Faso hadi Agosti 14 2015. Huu ni Mkutano wa Dunia, wa chama cha Wafanyakazi Wakristo, (MMTC), ambao kwa mwaka huu umefanyika kwa fadhila za wafanyakazi Wakristo wa Ouagadougou, na kuhudhuriwa na wajumbe wanachama kutoka Burkina Faso yenyewe, pia kutoka Benin, Ivory Coast, Cameroon, Ghana, Madagascar, Mali na Uganda. Mkutano unalenga kutoa azimio lake la mwisho kwa ajili ya ufanyaji upya jamii ya leo.
Kati ya yale yaliyo jadiliwa ni pamoja na kupambana na utofauti unaotokana na wengine
kusahaulika katika hatua za maendeleo ya jamii.. Mkutano huu ulifunguliwa kwa Ibada
ya Misa iliyoongozwa na Kardinali Philippe Ouédraogo, Askofu Mkuu wa Oaugadogou,
ambaye katika hotuba yake, alionyesha kuwa ujenzi wa mshikamano na udugu endelevu
ni ndoto ya kanisa kwa ajili ya kuleta umoja katika maisha ya kijamii. Kwa kufanya
hivyo, Kardinali alielezea matumaini yake kuwa, chama hiki cha Wakristo Wafanyakazi,
kitaweza saidia kupambana kutojali kwa matajiri ambao wana macho zaidi ya kuona yale
yanayowazunguka katika changamoto kubwa ya umaskini na ufukara.
Wengine waliokwisha toa mchango wao katika mkutano huu ni pamoja Timothée Ody, Rais
wa Uratibu wa Mmct Afrika: ambaye akilalamikia uwepo wa dunia iliyojaa dhulma, ubinafsi
na choyo. Hasa alisisitiza juu ya mwelekeo wa sasa wa uwepo wa siasa yenye kupoteza
hisia ya haki na dhidi ya mfumo wa kiuchumi ulio kinyume na haki za kijamii. Kwa
hiyo ametoa wito kwa jamii kuzingatia utendaji wa usawa na manufaa ya wote. "
Na Charo Castelló Alfaro, ambaye ni Mwenyekiti mwenza wa Mmct, yeye anasema,
inawezekana kabisa kuleta mabadiliko chanya duniani, iwapo jamii itazingatia kutekeleza
sera ya haki hasa katika ugawaji wa mali na haki za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.
Chama hiki cha Wakristo Wafanyakazi cha Dunia , kina wanachama wake katika nchi 79
za pande mbalimbali za dunia. Wazo la kuanzishwa kwa Chama hiki lilianzishwa kwa mara
ya kwnaza na wafanyakazi Wakristo wa Ujerumani, Austria, Ubelgiji, Ufaransa, Uholanzi
na Uswisi kwa lengo la kudumisha mafunzo, elimu na uinjilishaji, kwa mujibu wa mwongozo
wa mafundisho ya kijamii ya Kanisa. Chama kilichoanzishwa rasmi Roma, mwaka 1966,
sambamba na kumbukumbu ya mwaka wa 75 tangu Papa Leo XIII, alipoweka saini waraka
wa Rerum Novarum, uliolenga katika harakati za wafanyakazi, ajira, ukosefu wa ajira,
wastaafu na akina mama wa nyumbani.
Papa Leo XIII katika waraka wake huu wa Rerum Novarum, uliopelekwa kwa Wakuu wote
wa Kanisa, Maaskofu Maaskofu wakuu , Mapatriaki na wakuu wengine wa kiserikali wenye
kuwa na uhusiano naKiti kitakatifu hasa unazungumzia juu ya utendaji wa haki na wajibu
katika kazi.
Unalenga kutoa tafakari kwa ajili ya kufanya mabadiliko ya kiroho, kwa ajili ya kukomesha
uwepo wa vurugu na maonevu katika maeneo ya kazi .
All the contents on this site are copyrighted ©. |