Papa-ingawa miaka 70 imepita bado shambulio la Nyuklia Hiroshima na Nagasaki, linatisha
Jumapili mchana , Papa Francisko akiwahutubia mahujaji na wageni baada ya sala ya Malaika wa Bwana, katika hotuba yake pia alikumbuka tukio baya lililofanyika miaka 70 iliyopita, tarehe 6 na 9 Agosti 1945, mashambulio ya ndege za kivita, zilizomimina mabomu ya atomiki" juu ya mji wa Hiroshima na Nagasaki na kuteketeza miji hiyo. Papa alisema ni kumbukumbu ya kutisha, inayotoa wito kwa watu wote duniani, kukumbuka kuwaombea wote walioangamizwa na shambulio hili. Alikemea vikali matumizi ya silaha za nyuklia akisema ni lazima dunia iongeze juhudi zaidi katika kazi za kuelekea amani kamili, kwa kueneza maadili ya udugu, kupitia uwepo wa hali ya hewa ya mshikamano na amani miongoni mwa watu wote.
Papa alielezak wa kurejea tukio hilo, ambalo huko Nagasaki Ujapani, Jumapili watu walikusanyika, katika uwanja wa Amani wa Nagasaki, ambako kumbukumbu za kitaifa kwa ajili ya kupita miaka 70 tangu kutupwa kwa mabomu ya atomiki na Marekani, shambulio lililoua watu zaidi ya 80 elfu. Na Waziri Mkuu Abe wa Japan akihutubia mahali hapo aliitaka dunia kuachana na silaha za nyuklia.
All the contents on this site are copyrighted ©. |