2015-06-27 17:20:00

Madaktari na wauguzi, angalieni watu wanaishia kwa waganga wa kienyeji!


Ifuatayo ni hotuba iliyotolewa na Padre Reginald Mrosso, Mkuu wa Shirika la Wamissionari wa Damu Azizi ya Yesu, Vikarieti ya Tanzania wakati wa kuwaaga wanafunzi Wakatoliki wanaohitimu masomo ya utabibu na uuguzi, Chuo cha Utabibu na uuguzi, Mvumi, Dodoma, hapo tarehe 27 Juni 2015.

WAHESHIMIWA WAHITIMU WANACHUO WAKATOLIKI

Tumsifu Yesu Kristo!

Naomba nianze kwa kumshukuru Mungu Baba Mwenyezi na mweza wa yote kwa mapenzi yake kwetu na ninyi wahitimu –kwa heshima hii kubwa mliyonipa ya kujumuika nanyi katika siku hii muhimu na ya kihistoria ya mahafali yenu. Hongereni sana.

Nimefarijika sana kuwa miongoni mwa watu waliopata bahati ya kuishuhudia siku hii pamoja nanyi. Sote hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa huruma, kwa kutujalia uhai na afya njema na kutuwezesha kuwepo kushiriki katika sherehe muhimu katika maisha yenu na ya watu mtakaowahudumia. Hatuna budi pia kuwashukuru wote tukianzia tena na Mwenyezi Mungu mweza wa yote na wale wote waliowazesha katika hatua mbalimbali za maisha yenu hata mkawa jinsi mlivyo siku ya leo.

Mwanafalsafa Aristotle alisema mizizi ya elimu ni michungu lakini matunda yake ni matamu. Ninyi mmebahatika kupata elimu nzuri lakini muhimu sana na ambayo inawapa jukumu kubwa sana katika maisha ya watu na jamii. Mnashughulika na uzima na uhai wa mwanadamu. Tena ninyi ni wakristo kwa hiyo wajibu wenu unaongezeka zaidi na kudaiwa zaidi. Kwa maisha yenu na imani yenu mnashiriki moja kwa moja na Mungu katika kuulinda uhai na uzima. Hayo ni mapenzi makubwa mno ya Mungu Baba kwetu sisi. Kumbe Mungu Baba Mwenyezi ametupatia nafasi ya pekee ya kufanya kazi pamoja naye. Hata neno la Mungu siku ya leo – somo la kwanza na somo la pili –twasikia habari juu ya uhai na uzima:

Katika Mdo. 3:1-10 – twasoma habari juu ya uponyaji kwa jina la Yesu. .... Petro akasema, fedha na dhahabu mimi sina, lakini niliyo nayo ninakupa. Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, inuka na tembea. kisha Petro akamshika mkono wa kulia, akamwinua na mara nyayo zake na viungo vikaimarika, akaruka, akaweza kusimama na kutembea na kuruka ruka na kumsifu Mungu.

Kumbukeni daima kwamba uhai wa kweli hupatikana kama mkifanya kazi na Mwenyezi Mungu. Wewe jione kuwa ni chombo chake Mwenyezi Mungu na unashiriki katika mpango huo rasmi wa Mungu wa kulinda uhai na uzima. Mwenye uhai wa kweli ni Mungu tu, na wewe ujione kuwa chombo chake. Kanisa likitoa jibu la mahangaiko mbalimbali ya mwanadamu na maendeleo ya sayansi linalazimika daima kutoa mafundisho muhimu ambayo yanasimamia mapenzi yake Mwenyezi Mungu. Weledi huu mliopata na wajibu wenu kama wakristo utumike kuokoa maisha ya watu na kuimarisha hadhi ya mwanadamu.

Niwashirikishe barua ya Mwenyeheri Papa Paulo VI, ....... nanukuu

Humanae Vitae (Latin Of Human Life) is an encyclical written by Pope Paul VI and issued on 25 July 1968. Subtitled On the Regulation of Birth, it re-affirms the orthodox teaching of the Catholic Church regarding married love, responsible parenthood, and the continued rejection of most forms of birth control.

"On the Regulation of Birth":

Subtitled "On the Regulation of Birth," the encyclical begins by noting that "The transmission of human life is a most serious role in which married people collaborate freely and responsibly with God the Creator." The increase in global population, "a new understanding of the dignity of woman and her place in society, of the value of conjugal love in marriage and the relationship of conjugal acts to this love," and "man's stupendous progress in the domination and rational organization of the forces of nature" has raised "new questions" that "[t]he Church cannot ignore."

To Doctors and Nurses

27. Likewise we hold in the highest esteem those doctors and members of the nursing profession who, in the exercise of their calling, endeavor to fulfill the demands of their Christian vocation before any merely human interest. Let them therefore continue constant in their resolution always to support those lines of action which accord with faith and with right reason. And let them strive to win agreement and support for these policies among their professional colleagues. Moreover, they should regard it as an essential part of their skill to make themselves fully proficient in this difficult field of medical knowledge. For then, when married couples ask for their advice, they may be in a position to give them right counsel and to point them in the proper direction. Married couples have a right to expect this much from them. Mwisho wa kunukuu.

Mwanzilishi wa uuguzi wa kisasa na uimarishaji wa usimamizi na afya ya jamii, Bi Florence Nightingale – 1820 – 1910 - alijitoa bila kujibakiza katika kuwahudumia wagonjwa. Alifanya kazi sana na hivyo kubadili kabisa mwelekeo wa kazi hii kutoka kutokuwa ya kitaalamu na kuwa kazi ya kitaalamu- (medical profession) Hivyo zingatieni maadili ya kazi na ya taaluma ili muweze kuleta faraja ya kweli kwa wagomjwa mtakaowahudumia.

Igeni mifano ya mama huyu ambaye furaha yake ilipatikana katika kuwahudumia wagonjwa na wote wenye mahitaji ya afya ya mwili na kisaikolojia. Alihudumia wagonjwa wote kwa usawa bila kujali imani zao na hali zao za kiuchumi. Alitanguliza huduma kwa wagonjwa bila kujali yeye anapata mshahara kiasi gani.

Tumieni elimu mliyopata katika kufundisha watumishi wengine wa sekta ya afya ili muweze kuboresha kazi na taaluma ya uuguzi. Ninyi pia ni waalimu wa wagonjwa - wafundisheni na kuwaelekeza kwa upole ili waweze kufaidika na elimu mliyopata. Jengeni mazingira chanya katika mahali penu pa kazi, salimianeni kwa uchangamfu na onyeshaneni upendo kwa kuongea vitu chanya na kutiana moyo. Kuweni wabunifu ili muweze kubadilisha mazingira yenu na kuwa mahali pazuri zaidi pa kufanyia kazi.

Kumbuka kuwa kazi yako ni jina lako – Falsafa hii ni nzuri sana. Kwa kawaida mtu ye yote mjuzi hatambuliki kwa jina lake bali kwa kazi yake anayofanya. Mara nyingi watu hawana haja ya kujua jina lako ila wanapenda kujua na kutaja huduma zako na kwa kawaida mjuzi hutafutwa kwa kazi afanyayo au huduma atoayo, si kwa jina, bali kwa huduma ipatikanayo – yule mchoma mbuzi, yule mganga maarufu – labda yule pale general hospital, yule mchezaji mzuri, yule mchoma mahindi n.k. Mla nyama hutoa sifa kwa nyama nzuri na hana haja kujua ni ng’ombe yupi aliyechinjwa, hali kadhalika mnywa maziwa, hatoi sifa kwa ng’ombe mtoa maziwa bali husifia utamu na uzuri wa mazuri. Katika utendaji wako ikifikia hatua hiyo – ujue kuwa umefaulu katika kazi yako.

Mtakatifu Antonio Maria Zakaria – 1502 –1539 ambaye ni msimamizi wa matabibu awe changamoto kubwa kwenu. Katika umri wake wa miaka 37 tu hapa duniani amefanya mengi. Akiwa na miaka 22 tayari alikuwa na shahada ya udaktari. Lakini hii haikutosheleza haja yake ya kuwahudumia watu na akatamani kuwa karibu zaidi na watu na akaamua kuwa Padre akiwa na miaka 26 ili awafikie watu kwa ukaribu zaidi. Leo hii tunamkumbuka si kwa jina lake bali kwa kazi nzuri aliyofanya ya kuwahudumia watu kimwili na kiroho. Awe changamoto kwenu.

Wapo wasomi wengi watakatifu ambao mchango wao katika jamii umeleta maendeleo makubwa ya kimwili na kiroho – kina Mtakatifu Agostino wa Hippo, Thomas Aquinas, Albert Mkuu. Wapo watu mashuhuri pia ambao wametumikia jamii vizuri – Mwl. Julius Kambarage Nyerere na leo hii baadhi ya hao wengi – Baba Mtakatifu Francisko – mwenye masters degree in Chemistry n,k. Watu ambao pamoja na uwezo wao mkubwa kielimu wametoa mchango mkubwa kijamii. Hawakujivunia uwezo wao wa akili na taaluma.

Napenda niwashirikishe baadhi ya changamoto ambazo ningependa ziwe chachu ya utendaji wenu na ziwakune vichwa na mioyo yenu mnapojiandaa kuingia rasmi katika sekta ya tiba na afya. Ikiwezekana na nyingine nyingi zilizopo na mtakazokumbana nazo mzifanyie kazi.

Bahati mbaya sekta ya afya imeingiliwa na wajanja wachache – wauza dawa mbadala ambao wako wengi. Watu ambao hawana taaluma ya tiba lakini wamejiingiza kwenye fani hii. Angalieni vibao/matangazo mengi ya waganga wa kienyeji, wauza dawa mbalimbali kwenye mikusanyiko au makongamano, semina n.k. Je, hawa wauza dawa na wengine wa aina hiyo wana hata elimu msingi ya hicho wanachofanya? Ni nini hatima yake kwa afya ya mwanadamu? Mchezaji Diego Costa wa Atletico Madrid –pamoja na utaalamu wote wa Tiba huko Ulaya – alienda kwa mganga wa kienyeji na akiamini kuwa atapita tiba kwa haraka zaidi.

Watu wengi kutokuwa tayari kupima afya zao kwa hiari na kuishia kutumia dawa bila kuchunguza afya. Ukosekanaji wa elimu na huduma mbadala kwa wagonjwa/magonjwa yaliyokuwa yakionekana ni ya wengine kama nchi za ulaya – kisukari, shinikizo la damu, saratani, dengue n.k. Binafsi sioni juhudi ya pekee inayofanyika kuwaandaa kikamilifu wahudumu wapya katika eneo hili. Tatizo hili na ambalo ni kubwa katika jamii yetu – sasa linafanywa na wajasiriamali tu na pengine wataalamu wa tiba hawaonekani sana.

Namna ya kuzuia magonjwa ambukizi – inakuwaje mtu anajua kuwa maji yaliyosimama ni mazalio ya mbu lakini hayuko tayari kuangamiza maeneo hayo? Ninyi mmepata elimu ya tiba – naamini kuwa tukiishia tu katika kutoa dawa bila kutoa tiba ya mazingira na kusaidia mabadiliko ya namna yetu ya kuishi, lengo lenu litakuwa halijakamilika. Bi Florence Nightingale alishughulika pia na mazingira ili yawe safi na kuepuka maambukizi. Je katika elimu yenu mnasoma pia maswala ya kinga au mnasomo tu juu ya tiba na uuguzi? Swala la kinga kabla ya tiba linapewa kipaumbele gani katika elimu yenu?

Ukosefu wa mchango wa wasomi katika shughuli za kawaida na za kujitolea za kijamii-kuwasaidia wengine – wengi wenu humuonekani tena hasa baada ya hapa, baada ya kumaliza masomo yenu vyuoni na hasa pia kama shughuli hiyo haina mshiko - kwa mfano kwenye sekta ya michezo, malezi ya vijana, kujitolea kutoa elimu ya afya, ushiriki wenu wa karibu na viongozi wa kanisa n. k. Mtakatifu Antonio Maria Zakaria, somo wa matabibu awape changamoto. Kama mjuavyo alikuwa padre na daktari lakini alijihusisha sana na kazi na matendo ya huruma, akiwatembelea na kuwafariji wagonjwa na maskini mahospitalini na magerezani.

"Our present-day world will not be saved by those who aim to drug the spiritual life and reduce everything to a question of economics or material well-being,” (St. Josemaria Balaguer).

Wagonjwa wengi kutomaliza dosi au kutokutumia dosi sahihi au kwa usahihi.  Swala la ubunifu katika sekta ya afya – anayekumbuka ile filamu ya MISSION– Bud Spencer anacheza kama mmisionari huko Amerika ya Kusini – alikuwa akitoa tiba kwa wagonjwa wake wa meno – hakuwa na ganzi lakini alichokuwa anafanya ni kumpiga mgonjwa ngumi na akiwa kwenye kizunguzungu anamng’oa jino n.k. Na inaonekana mgonjwa anapona. Mwisho, nawashukuru sana kwa kunisikiliza na nawatakieni kila lililo jema mnapoaanza maisha ya kuwahudumia wagonjwa. Karibuni katika huduma. Mungu awabariki sana na sherehe njema. Hongereni sana.

 

Padre Reginald Mrosso, C.PP.S.








All the contents on this site are copyrighted ©.