2015-06-17 15:11:00

Papa Francisko kuongoza Mkutano wa Makardinali tarehe 27 Juni 2015


Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi tarehe 27 Juni 2015 majira ya asubuhi, anatarajiwa kuongoza masifu ya adhuhuri kwa ajili ya mkutano wa kawaida wa Makardinali ili kutolea maamuzi kwa baadhi ya Wenyeheri wanaotarajiwa kutangazwa kuwa Watakatifu. Kati yao ni Padre Vincenzo Grossi mwanzilishi wa Shirika la Watawa wa vituo vya michezo. 

Sr. Maria wa Bikira Maria mkingiwa dhambi ya Asili, Mama mkuu wa Shirika la Marafiki wa Msalaba na mwishoni ni Ludovico Martin, Mwamini mlei na Baba wa familia pamoja na Maria Azelia Guèrin, Mwamini mlei na Mama wa familia: hawa walikuwa ni mtu na mke wake, mashuhuda amini wa Injili ya Familia inayomwilishwa katika uhalisia wa maisha ya kila siku.

Taarifa hii imetolewa na Monsinyo Guido Marini, Mshereheshaji mkuu wa Ibada za Kipapa. Anawaalika Makardinali wanaoishi mjini Roma na wale ambao watakuwepo Roma katika kipindi hiki, kushiriki kikamilifu katika mchakato huu, utakaoongozwa na Baba Mtakatifu Francisko.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.