2015-05-23 15:30:00

Bikira Maria msaada wa Wakristo, Utuombee na kutusimamia!


Mama Kanisa kila mwaka ifikapo tarehe 24 Mei anaadhimisha Kumbu kumbu ya Bikira Maria msaada wa Wakristo, ambaye kunako mwaka 2001 alitangazwa kuwa ni Mama na msimamizi wa China. Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican, mwishoni mwa Juma ameadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro kwa ajili ya kuikumbuka na kuiombea Familia ya Mungu Barani Asia. Ibada hii imehudhuriwa na viongozi pamoja na wafanyakazi wa Gazeti la L’Osservatore Romano pamoja na kiwanda cha Uchapaji cha Vatican.

Katika mahubiri yake, Kardinali Parolin, amekazia Ibada kwa Bikira Maria, jambo msingi katika maisha na utume wa Mtakatifu Yohane Bosco, ambaye Mama Kanisa anaadhimisha Jubilei ya Miaka 200 tangu kuzaliwa kwake. Itakumbukwa kwamba, Siku kuu ya Bikira Maria msaada wa Wakristo ilianzishwa na Papa Pio wa VII kunako mwaka 1815. Kardinali Pietro Parolin amewataka waamini kujiaminisha mbele ya Bikira Maria msaada wa Wakristo, ili awasaidie kumtangaza na kumshuhudia Yesu duniani.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.