2015-05-05 08:45:00

Uchaguzi mkuu Burundi: Hali inaendelea kuwa tete zaidi!


Baraza la Maaskofu Katoliki Burundi linaendelea kulaani fujo, vurugu na ghasia zinazofanywa na watu wanaodai kung’atuka kwa Rais Pierrre Nkurunziza kutoka madarakani, baada ya kumaliza muda wa uongozi wake na kamwe asipindishe katiba ya nchi kwa ajili ya mafao yake binadamu. Wachunguzi wa mambo wanabainisha kwamba, hali ya hewa kisiasa nchini Burundi ni tete kutokana na waandamanaji kuendelea kupambana na vikosi vya ulinzi na usalama vinavyotumia mabomu ya kutoa machozi ili kuwasambaratisha waandamanaji ambao kwa sasa wana lengo la kuelekea mjini Bujumbura.

Mkataba wa Arusha, uliosaidia Burundi kuanza tena hija ya demokrasia, haki na amani, lakini sasa hali inaendelea kuwa mbaya, hasa wakati huu Burundi inapojiandaa kufanya uchaguzi mkuu ambao kwa kiasi kikubwa umegubwa na utata. Jeshi la Polisi Burundi linabainisha kwamba, vikosi vya ulinzi na usalama vinaendelea kuunga mkono Mkataba wa Arusha, uliositisha kinzani za kisiasa na mauaji ya watu wasiokuwa na hatia.

Viongozi wa kisiasa nchini Burundi wanahamasishwa kulinda na kuheshimu Katiba ya nchi ambao kimsingi ni sheria mama, ili amani, maridhiano na utulivu viweze kurejea tena miongoni mwa watu, vinginevyo, machafuko ya kisiasa yakianza sasa, haijulikani, lini yataweza kufikia ukomo wake, wanasema viongozi wa Kanisa. 

RAM.








All the contents on this site are copyrighted ©.