Baba Mtakatifu Francisko mapema Jumamosi hii amekutana na Rais Sergio Mattarella wa Jamhuri ya Italia, ambamo wameweza kubadilishana mawazo juu ya mambo mbalimbali yanayogusa jamii ya Italia. Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Papa kumpokea rasmi mjini Vatican, Rais Sergio Mattarella, tangu alipochaguliwa kuwa Rais wa Italia katika uchaguzi uliofanyika tarehe 3 Februari 2015.
Katika hotuba yake kwa Rais Sergio , Papa amesisitiza Italia kutosahau urithi wake wa Kikristo, katika shughuli zake zote za kimaendeleo na kisiasa na hasa kwa ajili ya udumishaji wa maelewano miongoni mwa raia wote wa Italia. Aidha Papa ametoa wito kwa Rais na taasisi zote za Italia, kusikiliza "kilio cha maumivu" ya vijana wengi ambao hawana kazi. Papa pia alitumaini, maonyesho ya Kimataifa yanayofanyika Milan “Expo 2015, itakuwa fursa nzuri ya kuchukua maamuzi yanayofaa kwa ajili ya utetezi wa mazingira.
Kukutana kwa viongozi hawa, Papa Francisko na Rais Mattarella, kunatajwa kuwa
ishara thabiti ya maelewano kati ya watu wa Italia na Jimbo Takatifu, kama Papa
alivyobaini, inarejesha upya neema hii ya ushirikiano wa tangu maamuzi yaliyotenganisha
majukumu na wajibikaji kati ya serikali ya Italia na Serikali ya Jiji la Vatican,
kama jambo muhimu, lililoonyesha uwepo wa haja ya kutengeneza mfumo mpya wa ushirikiano,
kwa ajili ya mema ya kawaida kwa watu wa Italia na serikali ya Jimbo la Papa. Papa
kwa upande mwingine, alibainisha, Kanisa linahitaji hali utulivu na amani miongozni
mwa jamii kwa ajili ya kutekeleza utume wake wa kiroho. Hali inayoweza kufanikishwa
na kukuzwa na mamlaka ya umma. Na kwamba, maendeleo ya jamii yenye wingi wa mchanganyiko
wa watu mbalimbali, haiwezi kudai kutoona hali halisi zenye kusukuma umuhimu wa
uwepo wa maendeleo ya kidini ya kweli, si tu yenye kulishwa na urafiki, lakini
katika kutambua wajibu wake katika ujenzi wa jamii tulivu,nyenye mshikamano na umoja..
Papa ameonyesha imani yake kwa Rais Mattarella, aliyekua ndani ya malezi ya Kikristo,
kwamba, ataweza kutoa mchango mkubwa katika kukuza mwendelezo wa utamaduni wa Kikristo,
msingi wa historia ya Italia na tabia ya watu wa Italia. Imani yenye kuwa utendaji
wa kazi wa kila siku kwa taasisi zake, zikionyesha sura na historia ya pekee na uwajibikaji
katika nyanja zote za maisha ya Waitaliano, tangu ndani ya familia shule ya kwanza
ya mshikamano na shule maadili, ambavyo husaidia kuijumuisha jamii katika utendaji
wake kama sehemu ya malezi msingi ya mtu.
Aidha Papa Francisko alitoa ombi kwa Rais Mattarella, kusikiliza kwa makini kilio
cha uchungu cha vijana wasiokuwa na ajira, akisema kati ya mazuri yote ya kimaendeleo,
ni muhimu juhudi zote za pamoja , kutambua kazi, katika umashuhuri wake wa kujenga
uhusiano wenye kuwa na utu sawa, na uwezekano wa kujenga maisha yenye heshima na
uhuru. Katika kukabiliana na changamoto hii, Papa anasema jumuiya ya kanisa, itafanya
kazi bega kwa bega, katika kupata ufumbuzi wa tatizo hili, kuwa kipaumbele katika
utafutaji wa haki. Kwa namna ya kipekee vijana wanahitaji kufanya kazi , ili waweze
kuwa na maisha ya utulivu, na hivyo kuondokana na vishawishi vya kuingia katika utendaji
usiofaa na majaribu yenye kuhatarisha usalama .
Aidha Papa katika hotuba yake , hakusahau kutoa shukurani zake kwa serikali ya Italia kwa juhudi inazofanya katika kuwapokea mamia ya wageni wahamiaji na wakimbizi wanaotafuta kusalimisha maisha yao. Papa amesema hii ni hazina kubwa kwa Italia katika kudumisha mila na utamaduni i wake, wenye kulishwa na kuvuviwa na imani ya Kikristo, kwa ajili ya kufanikisha maendeleo na maelewano, kama mchango wake katika sadaka ya kujenga amani na haki duniani.
All the contents on this site are copyrighted ©. |