2015-04-15 06:59:00

Mwaka wa Familia Jimbo kuu la Mwanza: Umuhimu wa Sakramenti za Kanisa


Askofu mkuu Thaddeus Ruwa’ichi wa Jimbo kuu la Mwanza katika barua yake ya kichungaji kwa ajili ya maadhimisho ya Mwaka wa Familia, anafafanua kwa kina na mapana dhana ya familia katika Maandiko Matakatifu na maudhui yanayokumbatia maisha ya sala na Sakramenti za Kanisa. Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican kama sehemu ya maandalizi ya maadhimisho ya Sinodi ya Familia, inaendelea kukuletea barua hii, ili kukusaidia wewe msikilizaji na msomaji kutambua mambo msingi katika maisha ya ndoa na familia, iwe uweze kuwa shuhuda wa Injili ya Familia.

Katika Makala hii, Askofu mkuu Ruwa’ichi anabainisha umuhimu wa Sakramenti ya Upatanisho katika maisha ya ndoa na familia. Hapa Wakristo wanahimizwa kuwa na ujasiri na unyofu wa kuzitambua dhambi, kuziungama na kujitahidi kuepuka nafasi za kutenda tena dhambi hizi baada ya kujipatanisha na Mungu pamoja na jirani zao.

Barua hii ya kichungaji inafafanua kwa kina na mapana maana ya Fumbo la Ekaristi katika maisha na utume wa Kanisa. Katika maadhimisho ya Mwaka wa Familia, Waamini wanaalikwa kwa namna ya pekee kabisa kutambua ukuu na utakatifu wa maadhimisho ya Sakramenti ya Ekaristi Takatifu. Waamini waachane na mazoea ya kuipokea Sakramenti hii kwa mazoea wala wakiwa katika dhambi ya mauti kwani wanakufuru. 

Jimbo kuu la Mwanza,

Tanzania.








All the contents on this site are copyrighted ©.