2015-03-03 09:28:26

Uchaguzi umefanyika katika mazingira ya amani!


Wasimamizi wa uchaguzi mkuu nchini Lesotho uliofanyika hivi karibuni kutoka Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Kusini mwa Afrika, IMBISA wanasema kwamba, uchaguzi ulikuwa huru na wa haki na kwamba, watu wengi wametumia haki yao ya kikatiba kutekeleza wajibu wao barabara katika hali ya amani na utulivu.

Waangalizi wa vituo vya kupigia kura kutoka kwenye vyama mbali mbali walisimamia zoezi hili kwa ufanisi mkubwa. Wajumbe kutoka IMBISA walikaribishwa kwa heshima na upendo, kila mahali walipotembelea ili kukagua zoezi zima la upigaji kura.

Baraza la Maaskofu Katoliki Lesotho katika barua yake ya kichungaji kama sehemu ya maandalizi ya uchaguzi mkuu, liliikumbusha Familia ya Mungu nchini Lesotho umuhimu wa kuweka mbele mafao ya wengi, umoja na mshikamano wa kitaifa badala ya kugubikwa na ubinafsi, uchu wa mali na madaraka; mambo ambayo yamekuwa ni chanzo cha majanga kwa nchi nyingi wakati na baada ya uchaguzi.







All the contents on this site are copyrighted ©.