Mama Kanisa anatufundisha kwamba, Moyo ndipo mahali ambapo nipo, ni kiini cha maisha
ya mwanadamu yaliyofichika, kisichoweza kufikiwa na akili ya kibinadamu, ni Roho ya
Mungu peke yake inayoweza kuupima na kuufahamu moyo. Moyo ni mahali pa uamuzi, penye
kina zaidi kuliko maelekeo yetu ya kiroho. Ndipo mahali pa kweli, pale ambapo mwanadamu
anachagua uhai au kifo.
Moyo ni mahali pa kukutania, kwa sababu kama sura
ya Mungu, mwanadamu anaishi katika mahusiano na maagano. Kumbe, moyo ni mahali patakatifu
sana panapotakiwa kulindwa na kutunzwa!
Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe
wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii anawakumbusha kwamba, moyo usiojua kupenda
unakuwa mgumu na kunyauka. Baba Mtakatifu anawaalika waamini na watu wote wenye mapenzi
mema kumwomba Mwenyezi Mungu awajalie moyo unaofahamu kupenda!
Na Padre Richard
A. Mjigwa, C.PP.S. Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.