2014-11-27 16:20:01

Ujumbe wa Papa kwa Kongamano la Kimataifa juu ya Miji Mkuu


Baba Mtakatifu Francisko, mapema Alhamisi hii alikutana na Makardinali na Maaskofu Wakuu kutoka Majiji na Miji Mkuu mbalimbali waliotoka mabara matano kwa ajili ya kushiriki katika Kongamano la Kimataifa lililofanyika Jumatatu Novemba 24, 2014, mjini Barcelona. Kongamano la Pili la Kimataifa kwa ajili ya kazi za Kichungaji katika Majiji na miji mikubwa duniani , kama ufuatiliaji wa Kongamano la kwanza lililofanyika Mei 20-22 2014. Washiriki wa Kongamano hili wakiwa ni pamoja na Maaskofu kutoka majiji na Miji Mkuu, pia wapo wataalam elimu ya maisha ya kijamii na Wanateolojia wanaoshughulika na masuala ya Kichungaji, wengi wao wakiwa ni Makardinali na Maaskofu Wakuu kutoka miji mikuu na miji mikubwa ya mabara matano.

Jumanne, Novemba 25, katika Kanisa kuu la FamiliaTakatifu la mjini Barcelona, Kongamano lilihitimiwa Mkutano wake, Lakini 27 Novemba, kulifanyika mkutano mwingine ulio hudhuriwa na Makardinali ishirini na tano na maaskofu wakuu kutoka miji mikubwa, mjini Vatican ambamo, Papa alikutano na washiriki wa Mkutano huo.

Papa katika hotuba yake alianza kuwashirikisha uzoefu wake w akuishi katika miji mikubwa wakati alipokuwa Askofu Mkuu wa Buenos Aris , mji wenye kuwa na wakazi karibia millioni 13. Ameitaja hii ni changamotokubwa kwa kanisa inayohitaji Uongozi katika Majiji na miji mikubwa, kubuni mbinu mpya za kukabiliana na mahitaji mengi ya kiroho, hii ni changamoto inayowaita kwenda mahali Mungu alipo

Papa amehimiza huku akirejea katika waraka wake wa Kichungaji wa Fraha ya Injili, ambamo alitoa angalisho katika kazi za kichungaji katika majiji na changamoto zake znyingi . Papa alieleza kwa kulenga katika mambo manne ambayo yanapaswa kufanyika ili kukabiliana na mahitaji ya mji mikubwa,akitaja kufanya mabadiliko katika fikira za kichungaji, kukubali kuwa na majadiliano na dini zingine, kuwa aminifu katika maisha ya kidini na kuwajali watu masikini.

Amemtaka kila mmoja kuendelea na juhudi zinazofanywa katika kutafakari, ya njia ya ubunifu, kwa jinsi gani inawezekana kufanikisha kazi ya uinjilishaji katika maeneo ya miji mikubwa, ambayo inazidi kupanuka kila siku. Jinsi ya kumfanya kila mtu kusikia hitaji la kutafuta kuwa karibu na huruma ya Mungu ambaye hamtekelezi mtu. Watu daima wajue kwamba Mungu anapatikana kila mahali. Wanachohitaji ni kuchukua hatua katika hisia ya maisha halisi, hasa katiak kuwafikia wale wanaojisikia kuwa wapweke, au wale waliopotoka au walio katika huzuni kubwa ya kujeruhiwa na hali za maisha , ambayo mara nyingi imesababishwa na jamii kujifungia yenyewe na kutotoa msaada kwa wahitaji na wenye shida.

Papa ametaja ni utume wa Kanisa kupeka habari Njema ya Wokovu wa Yesu Kristo na upendo wake wa kuokoa, katika mazingira tofauti, bila woga wa wingi wa vyama na bila kuanguka ndani ya ubaguzi wowote. Na bila ya kuona kama vile wameshindwa kufika vitongojini au kubadili mwelekeo kawaida, wakati inahitajika. Kanisa kama mama, daima hachoki kutafuta yaliyo mema kwa watoto wake , bila kupunguza nguvu na sadaka yake ya maisha , kamwe hachoki kuwamulikia mwanga wa Injili ya maisha yenye matumaini, furaha na amani; hata pale wanapokosa ujotojoto wa kujisikia kuunganishwa katika jamii, au katika mazingira ya kutengwa au uwepo ubaridi wa kutaja jina lake, lenye kukua ndani mwao kiroho katika mshikamano wa kweli na kila mtu, hasa masikini zaidi.

Papa Francisco ameeleza kuwatakia nia zao za Kichungaji kwa wakati huu , ziweze kumulikia utendaji wote wa Kanisa katika majiji na miji Mikuu.







All the contents on this site are copyrighted ©.