2014-11-27 15:38:00

Papa ahimiza ubunifu mpya, lakini kubaki aminifu katika karama za waanzilishi wa mashirika.


Tangu tarehe 25 -29 Novemba mjini Vatican , unaendeleshwa mkutano wa Shirika la Kipapa kwa ajili ya Taasisi za maisha yaliyowekwa wakfu na Vyama vya maisha ya Kitume chini ya Madambiu "Mvinyo Mpya katika viriba vipya: Kusikiliza njia ya Roho,kutambua na kuelekeza maisha wakfu, katika ubunifu aminifu katika imani. Lengo la Mkutano ni kukuza ubinifu aminifu katika wito maalum na karama ya kipekee ndani ya wito mpana wa maisha yaliyowekwa wakfu.

Baba Mtakatifu Francisko alikutana na washiriki wa Mkutano huu katika Ukumbi wa Clementina wa ndani ya Vatican. Hotuba yake,ilisisitiza uwajibikaji katika kazi zinazo waunganisha pamoja, kwa ajili ya kutathmini mvinyo mpya na upimaji wa ubora wa kiriba kipya , ziweze kuongozwa na vigezo katika uhalisi wa kiinjili kwenye kufanya uchaguzi, uaminifu wa karama, ubora wa huduma, pia angalisho kwa yaliyo madogo lakini nyeti, na heshima kwa utu wa kila mwanashirika na kila mtu..

Papa anasema, hakuna sababu ya kuwa woga katika kuachana kuacha viriba vizee, au kanuni za tangu kale na kuweka mvinyo katika viriba vipya, au kanuni mpya, ikiwa na maana ya kutohofia kufanya mabadiliko katika mifumo na taratibu za kale katika maisha ya kanisa na vivyo hiyo kwa maisha yaliyowekwa wakfu. Lakini ni lazima na muhimu kuzingatia ufahamu na maana ya mifumo ya kale , na kuiskiliza sauti ya Mungu,anavyopenda leo hii kazi zake zifanyike wakati Kanisa au mashirika au taasisi zinapo tembea katika hija ya kuuelekea ufalme wake hapa duniani.

Papa Francisco ameeleza na kutahadharisha dhidi ya kutumbukia katika miundo uongo na utetezi bandia unaotaka kufanya mabadiliko, lakini kumbe ni mitengo ya mwovu, inayooongoza katika tabia utengano, au wahusika kuwekwa mbali na kundi la wanakondoo waliotumwa kuwatumikia au kuzuia kusikiliza kilio cha wale wanaosubiri kwa hamu habari njema ya Yesu Kristo.







All the contents on this site are copyrighted ©.