2014-11-27 10:50:43

Nchi 13 zimefanikiwa kupambana na baa la njaa duniani!


Bwana Josè Graziano da Silva, Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa, FAO, Jumapili tarehe 30 Novemba 2014 anatarajiwa kutunuku vyeti maalum kwa nchi kumi na tatu ambazo zimefikia lengo la kupunguza baa la njaa kama sehemu ya utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Millenia, ifikapo mwaka 2015. Mkutano mkuu wa FAO kunako mwaka 1996 ulijiwekea lengo la kupunguza kwa kiasi kikubwa baa la njaa duniani ifikapo mwaka 2015.

FAO inasema kwamba, kuanzia mwanzoni mwa Mwaka 2014, nchi tatu zimejipambua katika mchakato wa kupambana na baa la njaa duniani, ingawa Mwaka 2013 nchi 38 zilionesha juhudi kubwa zaidi kwa kupunguza idadi ya wananchi wanaoteseka kwa baa la njaa. FAO inasema kwamba, Ethiopia, Gabon, Iran, Kiribati, Malaysia, Mauritania, Mauritius, Mexico na Ufilippini, zimefanikiwa kufikia lengo la kwanza kati ya Malengo ya Millenia la kupambana na baa la njaa na Brazil, Cameroon na Uruguay zimepunguza kiasi kikubwa cha wananchi wake wanaoteseka kwa baa la njaa.

Mkurugenzi wa FAO atatoa vyeti kwa wawakilishi wa nchi hizi, Jumapili ijayo kwenye Makao Makuu ya FAO yaliyoko mjini Roma.







All the contents on this site are copyrighted ©.