Ijumaa Papa kuanza ziara ya Kimtaifa ya Sita nchini Uturuki
Papa Francisco Ijumaa hii tarehe 28 Novemba 2014, anaanza ziara Kitume ya Sita kimataifa,
ambamo atakuwa Uturuki kwa siku tatu. Siku ya Jumatano, mara baada ya Katekesi yake,
Papa alitoa ombi kwa waumini,kwamba anahitaji sala na maombezi yao, ili kwamba,
ziara hii anayoifanya katika nafasi ya Petro , kumtembelea ndugu yake Andrea, iweze
kuzaa matunda ya amani, mazungumzo ya dhati kati ya dini na mapatano katika taifa
la Uturuki.
Ziara hii kitume ya siku tatu, inatajwa kuwa na maana kubwa katika
mtazamo wa kiekumeni na mahusiano ya kati ya dini. Ratiba ya ziara hii inaonyesha
kwamba, Ijumaa tarehe 28 Novemba , atakuwa Ankara, na kisha 29 na 30 Novemba, atakuwa
Istanbul ambako, atakutana Patriaki wa Kiekumeni, wa Constantinople, Bartholomew I,
kwa ajili ya kushiriki katika maadhimisho ya Sikukuu ya Mtakatifu Andrea.
Safari
ya Uturuki hivyo ni kuendeleza utamaduni ulioanzishwa na watangulizi wake kutembelea
Uturuki, na Patriaki wa Constantinople, ziara ya kwanza ilifanywa na Papa a Paulo
VI Julai 1967, na kisha Papa John Paul II, Novemba 1979, na Papa Benedict XVI, Novemba
2006. Msemaji wa Vatican Padre Federico Lombardi , akirejea ziara hii anasema ,
ni wazi nchi yoyote inayotembelewa na Papa, huwa makini na usalama wa ugeni huu. Na
ndivyo ilivyo sasa nchini Uturuki, kumekuwa na majadiliano na mikutano mingi baina
ya dini, kwa sababu Uturuki ni nchi yenye kuwa na Waislamu wengi, na kuna jumuiya
ndogo Wakatoliki. Na kama ilivyo siku zote wakati wa safari za Papa nchi za Nje,
huwa makini. Na katika ziara hii, Papa anakwenda kukutana na Mkuu wa Kanisa la Upatriaki
wa Kiekumeni wa Constatinople , Partiaki BartholewI, kama hatua ya maendeleo katika
mazungumzo ya kidugu na urafiki wa muda mrefu. Hivyo ziara hii itakuwa na tabia
za kiekumeni ambamo Papa atashiriki katika matumkiio mbalimbali muhimu ya kukutana
na watu mbalimbali kama ilivyoandaliwa na wenyeji wake. na akiwa mjini Istanbul,
ambamo kati ya mengine ataweka sahihi katika azimio la Pamoja . Ratiba kwa ujumla
inaonyesha kwamba, Ijumaa Papa Francisco baada ya kupokelewa kwa heshima za kitaifa
atatembelea jengo la makumbusho la Ataturki na kukutana na Rais a Jamhuri ya Uturuki
na viongozi wa kiserikali . Kwa siku ya Jumamosi, Papa ataelekea katika mji wa Ankra,
ambako atatembelea Jengo la Makumbusho la Mtakatifu Sofia. Msikiti wa Sultan Ahmet,
na atashiriki katika Ibada ya Kiekumeni katika Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu , na baadaye
kuwa na sala za kiekumeni katika Kanisa Kuu la Mtakatifu George na kukutana katika
hali ya faragha na Patriaki BartholewI Kwa Jumapili Papa kati ya mengine ataongoza
Ibada ya Misa katika hali ya faragha katika jengo la Uwakilishi wa Kitume. Na atakutana
na Rabbi Mkuu wa Uturuki , Isak Haleva, nakushiriki katika Ibada katika Kanisa la
Mtakatifu George ambalo ni muhimu katika Makainsa ya Kiotodosi. Papa atarejea
Vatican Jumapili jioni.