2014-11-26 14:51:13

Papa amteua Askofu Mpya wa Gikongoro, Rwanda


Baba Mtakatifu Francisko, amemteua kuwa Askofu mpya wa jimbo la Gikongoro, Rwanda, Padre Célestin Hakizimana, Padre wa Jimbo la Kigali, ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Rwanda.
Askofu Mteuli Célestin Hakizimana, alizaliwa Agosti 14 1963 katika Parokia ya Familia Takatifu ya Jimbo Kuu la Kigali. Baada ya masomo ya shule ya msingi alijiunga katika masomo ya seminari ndogo ya St. Vincent Rulindo (1977-1983) na kisha seminari ya Ndera (1983-1984). Mwaka 1985 aliingia seminari Propedeutico ya Rulindo na kumaliza masomo yake katika falsafa na teolojia katika Seminari Kuu ya Nyakibanda, Butare.
Alipadrishwa tarehe 21 Julai 1991. Pamoja na utume mbalimbali katika utumishi wa kanisa, kunako 2003-2010, alijiunga na masomo ya juu katika teolojia katika Chuo Kikuu cha Mtakaifu Tomas Naples, Italia , ambako alijipatia shahada ya uzamifu katika masomo ya teolojia. Na mwaka 2011, aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Rwanda.

Jimbo la Gikongoro liliundwa mwaka 1992, chini ya Jimbo Kuu la Butare. Iina eneo la kilomita mraba 2,057 kukiwa na jumla ya wakazi, 582 159 wenyeji, ambao zaidi kidogo yo (248,471) ni Wakatoliki. Kuna 13 parokia, zinazoongozwa na Mapadre 38 , kati yao 32 ni Mapadre wa Jimbo na 6 ni Mapadre watawa. Kuna Masista 70 na Waseminaristi 26.
Jimbo la Gikongoro, limekuwa halina Askofu tangu 2012, kufuatia kifo cha Askofu Augustin Misago, ambaye aliye tawala jimbo hilo kwa miaka 20 (1992-2012). Pongezi kwa Askofu mteule Celestinè Hakizimana.








All the contents on this site are copyrighted ©.