Kanisa ni mwendelezo wa safari yake kuekelea Ufalme wa Mbinguni - Papa
Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican, unatukumbusha sisi sote kwamba, Kanisa halina mwisho
lakini huendelea kutembea katika njia ya historia yake ya Ufalme wa Mbinguni, likiwa
mbegu na mwanzo wa safari hiyo. Ni maelezo ya Papa Francisko kwa mahujaji na wageni
waliokusanyika kusikiliza mafundisho yake Jumatano hii mjini Vatican.
Papa
alilenga katika historia ya safari ya wokovu , kwamba, safari hii itakamilika nyakati
za mwisho.... wakati ulimwengu utakapo badilika na kumezwa na furaha, amani na upendo
wa Mungu katika dunia ya kimbingu ya Yerusalem mpya.
Maelezo ya Papa pia yalilenga
katika mwendelezo wa uhusiano uliopo katika utendaji na umoja kati ya kanisa na dunia
na kanisa na Mbingu kupitia umoja na wale walio tutangulia kuondoka katika maisha
haya ya kimwili. Roho zilizo Mbinguni ambazo hutusaidia sisi kwa maombezi yao, wakati
sisi pia tunapoziombea roho zilizoko toharani, kupitia kazi za matendo mema, sala
na kushiriki katika Ibada ya Ekaisti.
Kama wana wa Kanisa, basi, tofauti si
kati ya wale waliokufa na walio hai , lakini zaidi ni kati ya walio ndani ya imani
ya Kanisa ya wale walio nje ya kanisa , watu wasioamini kwa Kristo. Mtakatifu Paulo
anatuambia sisi kwamba,si tu ubinadamu utakaowekwa huru dhidi ya maovu lakini viumbe
wote. Viumbe wote vitaweka huru katika ukamilifu, ukweli na uzuri wake.
Papa
ameutaja kuwa huo ni mpango wa Mungu kwa binadamu, katika kutembea kwenye njia ya
maisha, njia yenye msaada kwetu, na ishara ya furaha katika imani na matumaini ya
watu wote wanaosadiki kwa Mungu.