2014-11-22 07:46:26

Rais Napolitano wa Italia, ateta na Papa Francisko kwa faragha!


Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa tarehe 21 Novemba 2014 majira ya jioni akiwa kwenye Hosteli ya Mtakatifu Martha iliyoko mjini Vatican alikutana na kuzungumza na Rais Giorgio Napolitano wa Italia kwa faragha, ziara ambayo haikuwa kwenye ratiba ya shughuli za kawaida za Baba Mtakatifu kwa siku ya Ijumaa.

Padre Federico Lombardi anasema kwamba, mazungumzo haya ambayo yamedumu kwa takribani saa moja, yamefanyika katika hali ya urafiki na maelewano kati ya viongozi hawa wawili.







All the contents on this site are copyrighted ©.