Mh. Padre John Yaw Afoakwa, ateuliwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Obuasi, Ghana
Baba Mtakatifu Francisko, amemteua Mheshimiwa Padre John Yaw Afoakwa kuwa Askofu mpya
wa Jimbo Katoliki la Obuasi, Ghana. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mteule alikuwa ni
Gombera wa Seminari ya Jimbo la Obuasi, GHana. Alizaliwa tarehe 26 Januari 1955 hukoAkrokerry,
Jimbo Katoliki la Obuasi.
Baada ya masomo yake ya awali na sekondari alijiendeleza
katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana, kilichoko Roma, kunako mwaka 1983 na baadaye
aliendelea na masomo yake ya kidini na kuhitimu kunako mwaka 1986 na kuanza masomo
ya kitaalimungu katika Seminari kuu ya Mtakatifu Peter, iliyoko Cape Coast. Akajiendeleza
tena kwa masomo ya juu kwenye Chuo Kikuu cha Ghana, kilicho mjini Accra ambako alijipatia
shahada ya kwanza katika masomo ya jamii.
Baada ya majiundo yake ya kikasisi,
akapadrishwa kunako tarehe11 Julai 1992, akiwa ni Padre wa Jimbo la Kumas, Ghana.
Jimbo la Obuasi lilipozinduliwa, kunako mwaka 1995Askofu mteule Afoakwa akahamia jimboni
humo. Katika maisha yake kama Padre amewahi kuwa: Mwalimu na mhudumu wa wagonjwa;
Mkurugenzi wa Idara ya Katekesi Jimboni Obuasi, Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Gombera;
Paroko msaidizi na mwalimu wa shule kadhaa Jimboni mwake.
Hadi kuteuliwa kwake
na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Askofu mpya wa Jimbo Obuasi, Ghana alikuwa ni Gombera
wa Seminari ya Mtakatifu Louis, Jimboni Obuasi, Ghana.