2014-10-29 09:50:33

Rasilimali "kiduchu" imetolewa kupambana na Ebola


Bwana Christos Stylianides, Mratibu mkuu wa ugonjwa wa Ebola kutoka Jumuiya ya Ulaya anasema kwamba, kunahitajika jumla ya wataalam 40, 000 mapema iwezekanavyo ili kukabiliana na janga la ugonjwa wa Ebola, huko Afrika Magharibi. Wataalam hawa wanapaswa kupewa uhakika kwamba, wataweza kuondolewa katika maeneo watakayokuwa wanahudumia, kama hatari ikijitokeza na kwamba, yeye mwenyewe atasimamia operesheni ya kuokoa wananchi wa Ulaya ambao wameathirika kutokana na ugonjwa wa Ebola.

Bwana Stylianides anasema, Jumuiya ya Kimataifa haikuchukua hatua madhubuti kupambana na ugonjwa wa Ebola kisayansi tangu ulipojitokeza kwa mara ya kwanza na mapokeo yake, watu wakajikuta wanakumbatia imani potofu. Serikali ya Marekani inaendelea kuchukua tahadhari kubwa kwa watu wanaotoka katika maeneo ambayo yameathirika kwa ugonjwa wa Ebola, kwa kuwatenga kwa muda kabla ya kuanza maisha ya kawaida katika familia zao.

Australia imeamua kusitisha kutoa vibali vya kuingia nchini humo kwa wananchi wanaotoka katika nchi za Afrika Magharibi kama sehemu ya tahadhari ya kuenea kwa ugonjwa wa Ebola.







All the contents on this site are copyrighted ©.