2014-10-25 15:08:07

Kanisa linamshukuru Mungu kwa zawadi ya Askofu Josefu Mlola wa Jimbo Katoliki Kigoma


Askofu Desiderius Rwoma wa Jimbo Katoliki Bukoba ambaye pia ni msimamizi wa kitume wa Jimbo Katoliki Singida, katika mahojiano maalum na Radio Vatican anasema anapenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwajalia waamini wa Jimbo Katoliki la Kigoma mchungaji mkuu atakayewaongoza, wafundisha na kuwatakatifuza kadiri ya mapenzi ya Mungu. RealAudioMP3

Anamshukuru Baba Mtakatifu Francisko kwa kumteua Askofu Josefu Mlola, kwani hii inaonesha kwamba, ana mpango naye kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya Familia ya Mungu Jimboni Kigoma. Hii ni neema na baraka ambayo waamini na watu wote wenye mapenzi mema wanapaswa kuifurahia kwani hiki ni chombo cha Mungu kwa ajili ya kazi ya ukombozi. Kama kiongozi ana mapaji, karama na mapungufu yake, lakini Mungu amemwona kuwa ndiye anayehitaji kuliongoza Jimbo Katoliki la Kigoma.

Askofu Rwoma anawaalika watu kuendelea kumpongeza kwa njia ya sala pamoja na kumshika mkono, ili kazi hii mpya iweze kuzaa matunda ya toba, wongofu wa ndani na maendeleo kwa wananchi wa Kigoma katika ujumla wao.







All the contents on this site are copyrighted ©.