2014-10-19 11:12:00

Makatibu wakuu kutoka AMECEA wanakutana Bagamoyo!


Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania linatarajiwa kuwa ni mwenyeji wa mkutano mkuu wa pili wa Makatibu wakuu wa Mabaraza ya Maaskofu kutoka katika Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki na Kati, AMECEA. Mkutano huu unatarajiwa kufanyika katika mji mkongwe wa Bagamoyo, Jimbo Katoliki la Morogoro kuanzia tarehe 21 hadi tarehe 22 Oktoba 2014.

Mkutano huu utaongozwa na Padre Ferdinandi Lugonzo, Katibu mkuu wa AMECEA ambaye anafafanua kwamba, Makatibu wakuu kutoka AMECEA watapembua kwa kina na mapana mikakati ya utekelezaji wa maazimio yaliyotolewa na Mababa wa AMECEA katika mkutano wao wa kumi na nane uliofanyika mjini Lilongwe, Malawi. Mkutano huu unafutia mkutano mwingine wa Bodi tendaji ya AMECEA uliomalizika hivi karibuni.







All the contents on this site are copyrighted ©.