2014-10-19 10:50:30

Maisha ya wakimbizi na wahamiaji yako hatarini huko Mediterania


Shirika la kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa limeonesha wasi wasi wake kutokana na uamuzi wa Serikali ya Italia kusitisha operesheni maalum kwa ajili ya kuokoa maisha ya wakimbizi na wahamiaji baharini kwa kusema kwamba, maamuzi haya yataharisha zaidi maisha ya wakimbizi na wahamiaji ambao wanatafuta usalama na nafuu ya maisha Barani Ulaya.

Takwimu zinaonesha kwamba, tangu Oktoba 2013 hadi sasa kuna zaidi ya watu 150, 000 waliokolewa baharini kutokana na msaada a Serikali ya Italia. Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa linaziomba nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya kuunganisha nguvu zao katika operesheni ya kuokoa maisha ya wakimbizi na wahamiaji wanaotaka kuingia Barani Ulaya.

Kuanzia tarehe Mosi, Novemba, 2014, Serikali ya Italia itasitisha operesheni ya kuokoa wahamiaji na wakimbizi na zoezi hili sasa litafanywa na "Frontex" Wakala wa Wakimbizi kutoka Umoja wa Ulaya, ambao hadi sasa unalalama kukosa rasilimali vifaa na watu.







All the contents on this site are copyrighted ©.