Jumapili 28 Septemba katika uwanja wa Vatican, ulifurikwa na sura mbalimbali za wazee
kutoka pande zote za dunia, ambako Papa Francisko alikutana na wazee kaka ilivyokuwa
imeandaliwa na Baraza la Kipapa kwa ajili ya familia, kuadhimisha Siku Kuu ya Wazee,
iliyoitwa ” Baraka ya maisha marefu”. Papa mstaafu BenediktoXV1, alikuwa miongoni
mwao, ambapo Kabla ya adhimisho la Ibada ya Misa, Papa Francisko, alisikiliza baadhi
ya shuhuda za wazee na pia kuongea nao.
Alimshukuru Mwenyekiti wa Baraza la
Kipapa kwa ajili ya Familia, Askofu Mkuu Vincenzo Paglia kwa maandalizi haya ,vilevile
alipongeza pia Papa Mstaafu Benedikito XV1 kwa uwepo wake, na kwamba, mara nyingi
amefurahia kuona anaishi ndani ya Vatican. Amemwita kuwa babu mwenye hekima ndani
ya nyumba. Papa Francesko ameshangazwa na ushuhuda wa wazee wawili kutoka Iraq walioweza
kukimbia ghasia na vurugu, na kuita uwepo wao kuwa zawadi kwa kanisa.
Papa
Francisko alisema, vurugu dhidi ya wazee na watoto siyo kitendo cha kiutu, lakini
Mungu hawaachi wazee peke yao, huwapa msaada wake, ili waendelea kutoa kumbukumbu
kwa ajili yao na kwa ajili yetu , kwa sababu ni sehemu ya familia kubwa ya kanisa.
Imani yao ni kama mti unaoendelea kukua na kutoa matunda. Uzee ni kipindi cha neema
ambamo Bwana anatualika katika wito wake, kutunza na kuonyesha Imani, anatualika kusali
na hasa kuomba na kuwa karibu na wenye kuhitaji. Wazee wana uwezo wa kutambua hali
ngumu , na nguzo yao ni sala ambayo ina nguvu, alisema Papa.
Papa aliendelea
kuwaenzi babu na bibi kwamba, kwa namna ya pekee wamepokea baraka ya kuona watoto
wao (Zab 128,6) na wao wamekabidhiwa kazi kubwa ya kuonyesha uzoefu wa maisha, historia
ya familia katika Jumuiya ya watu. Babu ni “ Baba mara mbili”, na ndivyo ilivyo kwa
bibi “mama mara mbili” Tukikumbuka wito wa babu wa kuendeleza thamani ya urithi wa
Imani.
Papa Francisco kwa maneno hayo, alikumbuka ziara yake aliyoifanya
hivi karibuni nchini Albania na nchi nyingine zinazofanana na hiyo kwa kipindi cha
kidkteta ya kikomunisti, kwamba ni wazee waliofanya kubatiza watoto mafichoni , na
hivyo kuokoa imani ya watu hao.
Kwa nyakati hizi Papa Francisko alibainisha
kwamba siyo familia zote zinawapokea wazee, Na ndiyo maana ni vema kuwepo nyumba za
kuwapokea , lakini ziwe nyumba ukweli na wala zisiwe mahabusu, nyumba hizo iwe kwa
manufaa ya wazee na isiwe kwa manufaa mengine. Kwa mantiki hiyo Papa aliwashukuru
kwa wale wote wanaokwenda kuwatembelea wazee katika nyumba za kupokea wazee, na wote
wanatoa huduma kwao.Vile vile kwa vijana wengi wanao fanya kazi ya kuwafurahisha wazee
wenye nyuso za masikitiko , kurejea furaha ya maisha katika umri wao mkubwa. Papa
alisema kwamba kuna tatizo kubwa la kuwaacha wazee peke yao, akisema katika ukweli
hii ni sawa na eutanasia iliyojificha.
Matatizo ya utamaduni wa ubaguzi dhidi
ya watoto, vijana wasio kuwa na kazi, na wazee inasikitisha sana, hasa pale inapokuwa
kwa sababu za mipango ya kiuchumi na maisha. Papa alitaja ubaguzi huo ni nje ya utu
tena ni ubatili mtupu. Ni lazima kutanguliza utu na si fedha. Aliongeza na kumtaka,
kila mkristo, kupinga sumu ya utamaduni wa ubaguzi, na kuunda jamii tofauti, inayokaribisha
zaidi, yenye utu zaidi , na zaidi ya yote ambayo haiweki pembeni wadhaifu na wanyonge.
Watu
wasio tunza wazee , ni watu wasiokuwa na maisha endelevu , kwa sababu wanapoteza
kumbukumbu, na kupoteza mzizi: kila mkristo lazima atunze mzizi wa njia ya sala,
neno la Injili na matendo ya huruma. Papa alimalizia akitoa mfano kwamba vitu vizuri
katika maisha ya familia , na katika maisha ya binadamu ni kumbembeleza mtoto na kumwacha
mtoto abembelezwe na babu na bibi.
Homilia ya Papa kwa wazee, imekuwa
ni makutano yaliyojaa furaha ,amani na matumaini Baba Mtakatifu Francsiko,
baada ya kukutana na kubarizi na wazee, katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro
, aliingia katika hatua nyingine ambamo aliongoza Ibada ya Misa ya shukurani kwa Mungu
kwa majaliwa ya kukutana na wazee. Papa aliyaita makutano haya kuwa ni wakati uliojaa
furaha, imani na matumaini.
Katika homilia yake , alikumbusha juu ya Mama
Maria akiwa kijana, wakati huo binadamu yake Elizabeti alikuwa mzee , lakini kwa
huruma Mungu katika uzee wao, Zakaria na Elizabeti , wakajaliwa mtoto. Kwa njia hii
Mama Maria anatuonyesha njia , ya kwenda kukutana na wazee ndugu zetu, kukaa nao,
kuwasaida, na zaidi kujifunza kutoka kwao , kwani wazee wana hekima na busara ya
maisha.
Papa alieleza na kwa kuyarejea masomo ya Siku akianza na somo la kwanza,
akisema, lilionyesha kana kwamba linaongelea juu ya amri ya nne ya Mungu, isemayo
waheshimu baba na mama upate miaka mingi na heri duniani ambayo Bwana Mungu amekupatia
(Kut 20,12) Hakuna maisha ya endelevu ya watu kama hakuna makutano na kizazi kipya
, iwapo hakuna watoto wanaopokea ushuhuda wa maisha ya wazazi wao. Pamoja na shukrani
za utambuzi kwa wazazi walio tupatia maisha haya, hatuna budi kumshukuru Baba Mungu
aliye mbinguni. Aliongeza Papa.
Papa Francisco aliangalisha vijana wa kizazi
hiki kwa sababu ya tamaduni na kwamba wanatofautiana na kizazi kilichopita, aliwataka
wawe makini katika uhuru wa chaguzi, ni lazima kuutauta ukweli na siyo chaguzi potofu
zinazoongozwa na uchu wa fedha, tamaa na madaraka.
Papa aliendelea kutafakari
juu ya somo la pili kutoka waraka Mtakatifu Paulo wa Timotea, akiielekea jumuiya
ya wakristo, kwamba Yesu hakutengua sheria katika familia , kati ya kizazi , bali
alileta ukamilifu. Bwana aliunda familia mpya, ambayo imeungana kwa ajili ya kufanya
mapenzi ya Mungu Baba. Upendo wa Yesu kwa baba yake unaleta ukamilifu wa upendo wa
wazazi wake na, ndugu zake , babu zake na kurudisha upya ndani ya familia kiini cha
Injili na Roho Mtakatifu. Kwa namna hiyo Mtakatifu Paulo anamsihi Timoteo ambaye ni
mchungaji na kwa maana hiyo baba wa Jumuiya , kuwa na heshima ya wazazi na familia
, na kumsihi pia awe na maelewano kama watoto. Babu ni kama Baba na bibi kama mama
(1Tm 5,1).
Mapenzi ya Mungu ni kwa watu wote hata Mkuu wa Jumuiya, na zaidi
ya hayo upendo wa Kristo unamsukuma afanye hivyo kwa upendo mkubwa. Kama vile Bikira
Maria alivyofanya japokuwa aliitwa kuwa Mama wa Masiya, lakini anajisikia kusukumwa
na upendo wa Mungu , ambamo ameupokea na kukimbia kumtembelea Elizabeti.
Ukirudi
katika picha iliyojaa furaha ,imani, matumaini na upendo , unaweza kufikiria Bikira
Maria akiwa nyumbani mwa Elizabeth, aliwasikia Zakaria na mkewe wakisali zaburi
yenye maneno kama “Ee Bwana Mungu ndiwe tumaini langu tokea ujana wangu,… usinitupe
wakati wa uzee wangu , nguvu zangu zipungukapo usiniache…Na hata nikiwa ni mzee mwenye
mvi, Ee Mungu usiniache. Hata niwaeleze wat u wa kizazi nguvu zako, na kila atakayekuja
uweza wako”. (71,5.9.18).
Kijana Maria alisikiliza , na yote akayaweka katika
moyo wake, Hekima ya Elizabeth na Zakaria , imetajirisha moyo wa binti Maria; licha
kwamba hawakuwa na uzoefu wa kuwa baba au mama, kwa sababu hata wao ilikuwa ni kwa
mara yao ya kwanza, lakini walikuwa na ujuzi wa imani, ujuzi kwa Mungu , ujuzi katika
matumaini yanayotoka kwa Mungu, na kwa namna hiyo ndiyo maana dunia inahitaji ujuzi
huo kila wakati. Maria alitambua manufaa ya kuwasikiliza wazazi wazee kwa hekima
yao na ikawa tunu kwake katika safari yake kama mwanamke na kama mama. Papa alimalizia
kwamba Bikira Maria anatuonyesha njia ya kukutana kati ya vijana na wazee. Msingi
wa siku zijazo unategemea na kuhitaji hatua hiyo ya kukutana.Vijana wanawapa nguvu
wazee katika safari ya maisha hati hatima yake, vilevile wazee kwa hekima zao huwatia
nguvu vijana katika safari yao ya maisha.