2014-09-23 08:34:17

Hakuna sayari nyingine ya kukimbilia


Jumapili 21Septemba yalifanyika maandamano makubwa katikati ya jiji la New York, Marekani, yakiwa na lengo la kupaza sauti juu ya madhara ya mabadiliko ya tabianchi. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon alishiriki maandamano hayo akijumuika na wananchi wote wakiwemo viongozi mashuhuri , na wanasiasa .

Taarifa kutoka Radio ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa Bwana Ban Ki Moon alisema hakuna kinachotegemewa kufanyika zaidi ya mpango wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na zaidi ya kuchukua hatua ambazo tayari zimeisha bainishwa. Alisitiza hakuna sayari nyingine ya dunia ya binadamu kukimbilia na hivyo ni lazima kushirikiana na kuchukua hatua stahili.

Athari za mabadiliko ya tabianchi ni pamoja na kuongezeka kwa kiwango cha maji ya bahari, majanga ya asili na ongezeko la kiwango cha joto.

Maandamano ya jumapili yamefanyika siku mbili tu kabla ya mkutano wa Katibu Mkuu kuhusu tabianchi kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

Mkutano huo utawaleta pamoja zaidi ya viongozi wa nchi 120, ili kuweka msukumo wa kufikia mkataba wa kimataifa kuhusu mbinu za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Inatarajiwa kuwa mkataba huo utafikiwa mjini Paris, Ufaransa hapo mwakani.

Idadi kubwa ya watu kukosa chakula haikubaliki:Vichi De Marchi
RipotI kuhusu wasiwasi wa ukosefu wa chakula duniani iliyowakilishwa hivi karibuni mjini Roma inaonyesha ukweli wa vitu viwili , kwanza kupungua kwa watu milioni 200 katika miaka 20 , na vilevile ukosefu wa chakula wa watu zaidi ya milioni 800.

Idadi hii hakubaliki alisema Bwana Vichi De Marchi mwakilishi wa Italia katika idara ya Mpango na chakula wa Dunia ,alisema iwapo wenye njaa hasa katika sehemu za Kusini mwa Afrika na Asia , inabidi siasa kuingilia kati.

Nchi ambazo zimeweza kupambana na tatizo la njaa, ndizo zimekuwa mstari wa mbele kuchagua njia ya kisiasa ili kutoa kipaumbele kukabiliana na tatizo hili, aliongeza Bwana Vichi.

Vilevile waziri wa siasa katia masuala ya kilimo, chakula na misitu Bi Martina Maurizio aliongezea kwamba katika mpango huo iwapo umoja wa Ulaya unataka ushindi juu ya changamoto hii inapaswa iwe na ujasiri. Hata hivyo Italia inajitahidi kufanya kila njia ikitumia matukio kama ya Expo ya Milan, kama njia mojawapo ya kutafuta mwafaka kamili .

Wito wa Waziri Martina unasema,pamoja na kusubiri wanasiasa kutekeleza wajibu wao, kila mwananchi anaweza kutoa mchango wake mdogo kama ule wa kuwa na umakini katika matumizi mabaya ,au uharibifu wa vyakula, jambo ambalo kwa nchi zilizoendela limekuwa tatizo sugu.

Akiongeza Mkufunzi wa siasa-kilimo na mwanzilishi wa (Last Minute Market) chombo kinachohusu namna ya kuokoa vyakula alisema kwamba; inasaidia nini kuongeza uzalishaji wa chakula asilimia 70% iwapo robo tatu ya chakula kinatumika hovyo? Aliwataka watu wote watafakari.









All the contents on this site are copyrighted ©.